Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 109

109
Sala ya Uthibitisho na Kutaka Kisasi
Kwa mwimbishaji. Ya Daudi. Zaburi.
1 # Zab 83:1 Ee Mungu wa sifa zangu, usinyamaze,
2Kwa maana wamenifumbulia kinywa;
Kinywa cha mtu asiye haki, cha hila,
Wamesema nami kwa ulimi wa uongo.
3 # 1 Sam 19:4,5; Zab 35:7,20; Yn 15:25 Naam, kwa maneno ya chuki wamenizunguka,
Wamepigana nami bure.
4Badala ya upendo wangu wao hunishitaki,
Ijapokuwa naliwaombea.
5 # Zab 38:20 Wamenichukuza mabaya badala ya mema,
Na chuki badala ya upendo wangu.
6Uweke mtu mkorofi juu yake,
Mshitaki asimame mkono wake wa kuume.
7 # Mit 28:9 Katika kuhukumiwa ataonekana hana haki,
Na sala yake itadhaniwa kuwa ni dhambi.
8 # Mdo 1:20 Siku zake na ziwe chache,
Usimamizi wake na atwae mtu mwingine.
9 # Kut 22:24; Yer 18:21 Wanawe na wawe yatima,
Na mkewe na awe mjane.
10 # Mwa 4:12 Kutanga na watange wanawe na kuomba,
Watafute chakula mbali na mahame yao.
11 # Ayu 18:9 Mdai na anase vitu vyote alivyo navyo,
Wageni na wateke mapato ya kazi yake.
12Asiwe na mtu wa kumfanyia fadhili,
Wala mtu wa kuwahurumia yatima wake.
13 # Zab 37:28; Mit 10:7 Wazao wake waangamizwe,
Jina lao likafutwe katika kizazi cha pili.
14 # Kut 20:5; Neh 4:5 Uovu wa baba zake ukumbukwe mbele za BWANA,
Na dhambi ya mamaye isifutwe.
15 # Ayu 18:17 Ziwe mbele za BWANA daima,
Aliondoe kumbukumbu lao duniani.
16Kwa kuwa hakukumbuka kutenda fadhili,
Bali alimfukuza mnyonge na mhitaji,
Hata akamfisha mtu aliyevunjika moyo,
17Naye alipenda kulaani, nako kukampata.
Hakupendezwa na kubariki, kukawa mbali naye,
18Alijivika laana kana kwamba ni vazi lake.
Ikamwingilia moyoni kama maji,
Na kama mafuta mifupani mwake.
19Na iwe kwake kama vazi ajivikalo,
Na kama mshipi ajifungao daima.
20Ndiyo malipo ya washitaki wangu toka kwa BWANA,
Na ya hao wanaoisingizia nafsi yangu mabaya.
21Na Wewe, MUNGU, Bwana, unitendee kwa ajili ya jina lako,
Kwa kuwa fadhili zako ni njema uniokoe.
22Kwa maana mimi ni mnyonge na mhitaji,
Na moyo wangu umejeruhi ndani yangu.
23Ninapita kama kivuli kianzacho kutoweka,
Ninapeperushwa kama nzige.
24 # Ebr 12:12 Magoti yangu yamedhoofu kwa kufunga,
Na mwili wangu umekonda kwa kukosa mafuta.
25 # Isa 37:22; Mt 27:39; Mk 15:29 Nami nalikuwa laumu kwao,
Wanionapo hutikisa vichwa vyao.
26Ee BWANA, Mungu wangu, unisaidie,
Uniokoe sawasawa na fadhili zako.
27 # Ayu 37:7 Nao wakajue ya kuwa ndio mkono wako;
Wewe, BWANA, umeyafanya hayo.
28 # Hes 22:12; Isa 65:14 Wao walaani, bali Wewe utabariki,
Wameondoka wao wakaaibishwa,
Bali mtumishi wako atafurahi.
29Washitaki wangu watavikwa fedheha,
Watajivika aibu yao kama joho.
30Nitamshukuru BWANA kwa kinywa changu,
Naam, nitamsifu katikati ya mkutano.
31Maana atasimama mkono wa kuume wa mhitaji
Amwokoe na wanaoihukumu nafsi yake.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 109: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia