Zab 110
110
Hakikisho la Ushindi kwa Mteule wa Mungu
Ya Daudi. Zaburi.
1 #
Zab 45:6; Mt 22:44; Mk 12:36; Lk 20:42-43; 1 Kor 15:25; Mdo 2:34-35; 1 Kor 15:25; Efe 1:20-22; Kol 3:1; Ebr 1:13; 8:1; 10:12-13 Neno la BWANA kwa Bwana wangu,
Uketi mkono wangu wa kuume,
Hata niwafanyapo adui zako
Kuwa chini ya miguu yako.
2BWANA atainyosha toka Sayuni
Fimbo ya nguvu zako.
Uwe na enzi kati ya adui zako;
3 #
Amu 5:2; Zab 96:9; Mdo 2:41 Watu wako wanajitoa kwa hiari,
Siku ya uwezo wako;
Kwa uzuri wa utakatifu,
Tokea tumbo la asubuhi,
Unao umande wa ujana wako.
4 #
Hes 23:19; Zek 6:13; Ebr 5:6; 6:20; 7:17,21 BWANA ameapa,
Wala hataghairi,
Ndiwe kuhani hata milele,
Kwa mfano wa Melkizedeki.
5 #
Zab 16:8; 2:5; Rum 2:5; Ufu 11:18 Bwana yu mkono wako wa kuume;
Ataseta wafalme,
Siku ya ghadhabu yake.
6 #
Hab 3:13
Atahukumu kati ya mataifa,
Ataijaza nchi mizoga;
Ataseta kichwa katika nchi nyingi.
7 #
Isa 61:1; Yn 3:34; Isa 53:12 Atakunywa maji ya mto njiani;
Kwa hiyo atakiinua kichwa chake.
Iliyochaguliwa sasa
Zab 110: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.