Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 2

2
Ahadi ya Mungu kwa Mtiwa Mafuta Wake
1 # Mdo 4:25-26 Mbona mataifa wanafanya ghasia,
Na makabila wanatafakari ubatili?
2 # Zab 45:7; Yn 1:41 Wafalme wa dunia wanajipanga,
Na wakuu wanafanya shauri pamoja,
Juu ya BWANA,
Na juu ya masihi#2:2 Au, mtiwa mafuta. wake,
3 # Lk 19:14 Na tuvipasue vifungo vyao,
Na kuzitupia mbali nasi kamba zao.
4 # Zab 11:4 Yeye aketiye mbinguni anacheka,
Bwana anawafanyia dhihaka.
5Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake,
Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake.
6Nami nimemweka mfalme wangu
Juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.
7 # Mdo 13:33; Ebr 1:5; 5:5; Mt 8:29 Nitaihubiri amri; BWANA aliniambia,
Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.
8 # Dan 7:13,14; Yn 17:4,5 Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako,
Na miisho ya dunia kuwa milki yako.
9 # Ufu 2:26-27; 12:5; 19:15; Mt 21:44 Utawaponda kwa fimbo ya chuma,
Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.
10Na sasa, enyi wafalme, fanyeni akili,
Enyi waamuzi wa dunia, mwadibiwe.
11Mtumikieni BWANA kwa kicho,
Shangilieni kwa kutetemeka.
12 # Yn 5:22,23; Yer 17:7 Shikeni yaliyo bora#2:12 Au, Pokeeni mafundisho au, Mbu suni Mwana., asije akafanya hasira
Nanyi mkapotea njiani,
Kwa kuwa hasira yake itawaka upesi;
Heri wote wanaomkimbilia.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 2: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia