Zab 45:9-17
Zab 45:9-17 SUV
Binti za wafalme wamo Miongoni mwa akina bibi wako wastahiki. Mkono wako wa kuume amesimama malkia Amevaa dhahabu ya Ofiri. Sikia, binti, utazame, utege sikio lako, Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako. Naye mfalme atautamani uzuri wako, Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie. Na binti Tiro analeta kipawa chake, Nao matajiri wa watu watajipendekeza kwako. Binti mfalme yumo ndani ana fahari tupu, Mavazi yake ni ya nyuzi za dhahabu. Atapelekwa kwa mfalme Na mavazi yaliyofumwa kwa uzuri. Wanawali wenzake wanaomfuata, Watapelekwa kwako. Watapelekwa kwa furaha na shangwe, Na kuingia katika nyumba ya mfalme. Badala ya baba zako watakuwapo watoto wako, Utawafanya kuwa wakuu katika nchi zote. Jina lako nitalifanya kuwa kumbukumbu Katika vizazi vyote. Kwa hiyo mataifa watakushukuru Milele na milele.