Zab 53
53
Kushutumiwa kwa Wasiomwamini Mungu
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Mahalathi. Utenzi wa Daudi.
1 #
Rum 3:10-12; Zab 10:4 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu;
Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza,
Hakuna atendaye mema.
2 #
Zab 33:13; 2 Nya 15:2 Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu,
Aone kama yuko mtu mwenye akili,
Amtafutaye Mungu.
3 #
Mhu 7:29
Kila mtu amepotoka, wameoza wote pamoja,
Hakuna atendaye mema,
La! Hata mmoja.
4 #
Yer 4:22
Je! Wafanyao maovu hawajui?
Walao watu wangu kama walavyo mkate,
Hawakumwita MUNGU.
5Hapo waliingiwa na hofu pasipokuwapo hofu,
Maana Mungu ameitawanya mifupa yake aliyekuhusuru.
Umewatia aibu,
Kwa sababu MUNGU amewadharau.
6Laiti wokovu wa Israeli utoke katika Sayuni!
MUNGU awarudishapo wafungwa wa watu wake;
Yakobo atashangilia,
Israeli atafurahi.
Iliyochaguliwa sasa
Zab 53: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.