Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 62

62
Wimbo wa Kusifia Imani kwa Mungu Pekee
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi.
1Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa kimya,
Wokovu wangu hutoka kwake.
2Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,
Ngome yangu, sitatikisika sana.
3 # Isa 30:13 Hata lini mtamshambulia mtu,
Mpate kumwua ninyi nyote pamoja?
Kama ukuta unaoinama,
Kama kitalu kilicho tayari kuanguka,
4 # Zab 28:3 Hufanya shauri kumwangusha tu katika cheo chake;
Huufurahia uongo.
Kwa kinywa chao hubariki;
Kwa moyo wao hulaani.
5 # Mik 7:7,10 Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa kimya.
Tumaini langu hutoka kwake.
6Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,
Ngome yangu, sitatikisika sana.
7 # Yer 3:23 Kwa Mungu wokovu wangu,
Na utukufu wangu;
Mwamba wa nguvu zangu,
Na kimbilio langu ni kwa Mungu.
8 # 1 Sam 1:15; Zab 42:4 Enyi watu, mtumainini sikuzote,
Ifunueni mioyo yenu mbele zake;
Mungu ndiye kimbilio letu.
9Hakika binadamu ni ubatili,
Na wenye cheo ni uongo,
Katika mizani huinuka;
Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili.
10 # Isa 26:4; Mk 10:23; Lk 12:15 Msiitumainie dhuluma,
Wala msijivune kwa unyang’anyi;
Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.
11Mara moja amenena Mungu;
Mara mbili nimeyasikia haya,
Ya kuwa nguvu zina Mungu,
12 # Ayu 34:11; Yer 17:10; Mt 16:27; 1 Pet 1:17; Rum 2:6; Ufu 2:23 Na fadhili ziko kwako, Ee Bwana;
Maana ndiwe umlipaye kila mtu
Sawasawa na haki yake.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 62: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia