Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 64

64
Sala ya Ulinzi kutoka kwa Adui
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu;
Unilinde uhai wangu na hofu ya adui.
2 # Zab 143:9 Utanificha mbali na shauri la siri la watenda mabaya,
Mbali na ghasia ya watu wafanyao maovu;
3 # Zab 57:4 Waliounoa ulimi wao kama upanga,
Wameielekeza mishale yao, maneno ya uchungu,
4Wapate kumpiga mkamilifu faraghani,
Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi.
5Walijifanya hodari katika jambo baya;
Hushauriana juu ya kutega mitego;
Husema, Ni nani atakayeiona?
6Hutunga maovu; husema, Tumefanya shauri kamili;
Na mawazo ya ndani ya kila mmoja wao,
Na moyo wake, huwa siri kabisa.
7Kwa hiyo Mungu atawapiga shabaha,
Kwa mshale mara watapigwa.
8 # Mit 12:13 Ndivyo watakavyokwazwa,
Ulimi wao wenyewe ukishindana nao.
Wote wawaonao watatikisa kichwa.
9Na watu wote wataogopa,
Wataitangaza kazi ya Mungu,
Na kuyafahamu matendo yake.
10 # Zab 32:11; Flp 4:4 Mwenye haki atamfurahia BWANA na kumkimbilia,
Na wote wenye moyo wa adili watajisifu.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 64: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia