Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 81

81
Ombi la Mungu kwa Waisraeli Wakaidi
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Gitithi. Ya Asafu.
1Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha,
Mshangilieni Mungu wa Yakobo.
2Pazeni zaburi, pigeni matari,
Kinubi chenye sauti nzuri, na kinanda.
3 # Hes 10:10 Pigeni panda mwandamo wa mwezi,
Wakati wa mbalamwezi, sikukuu yetu.
4 # Law 23:24; Hes 10:10 Kwa maana ni sheria kwa Israeli,
Ni hukumu ya Mungu wa Yakobo.
5Aliamuru iwe ushuhuda katika Yusufu,
Alipoondoka juu ya nchi ya Misri;
Maneno yake nisiyemjua naliyasikia.
6Nimelitenga bega lake na mzigo,
Mikono yake ikaachana na kikapu.
7 # Kut 17:7; Hes 20:13 Katika shida uliniita nikakuokoa;
Nalikuitikia katika sitara ya radi;
Nalikujaribu penye maji ya Meriba.
8Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya,
Ee Israeli, kama ukitaka kunisikiliza;
9 # Kut 20:2-3; Kum 5:6-7 Usiwe na mungu mgeni ndani yako;
Wala usimsujudie mungu mwingine.
10 # Zab 37:3; Yn 15:7 Mimi ndimi BWANA, Mungu wako,
Niliyekupandisha toka nchi ya Misri;
Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza.
11Lakini watu wangu hawakuisikiliza sauti yangu,
Wala Israeli hawakunitaka.
12 # Mdo 7:42; Rum 1:24 Nikawaacha wakaenda kwa ukaidi wa mioyo yao,
Waenende katika mashauri yao.
13 # Kum 5:29; Isa 48:18; Yer 44:4,5; Mt 23:37 Laiti watu wangu wangenisikiliza,
Na Israeli angeenenda katika njia zangu;
14Ningewadhili adui zao kwa upesi,
Na juu ya watesi wao ningegeuza mkono wangu;
15Wamchukiao BWANA wangenyenyekea mbele zake,
Bali wakati wao ungedumu milele.
16Naam, ningewalisha kwa unono wa ngano,
Ningewashibisha kwa asali itokayo mwambani.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 81: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia