Zab 82
82
Ombi la Kupata Haki
Zaburi ya Asafu.
1 #
Mhu 5:8; Kut 21:6 Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu;
Katikati ya miungu anahukumu.
2 #
Kum 1:17; Zab 58:1,2 Hata lini mtahukumu kwa dhuluma,
Na kuzikubali nyuso za wabaya?
3Mfanyieni hukumu maskini na yatima;
Mtendeeni haki aliyeonewa na fukara;
4Mwokoeni maskini na mhitaji;
Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.
5 #
Zab 11:3
Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani;
Misingi yote ya nchi imetikisika.
6 #
Ayu 21:32; Eze 31:14; Yn 10:34 Mimi nimesema, Ndinyi miungu,
Na wana wa Aliye juu, nyote pia.
7Lakini mtakufa kama wanadamu,
Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.
8 #
Zab 2:8; Ufu 11:15 Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi,
Maana Wewe utawarithi mataifa yote.
Iliyochaguliwa sasa
Zab 82: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.