Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Amosi 5:1-9

Amosi 5:1-9 SRUV

Lisikieni neno hili nilitamkalo liwe maombolezo juu yenu, enyi nyumba ya Israeli. Bikira wa Israeli ameanguka; hatainuka tena; Ameangushwa katika nchi yake; hakuna mtu wa kumwinua. Kwa kuwa Bwana MUNGU asema hivi; Mji uliotoka nje wenye watu elfu moja, utabakiziwa watu mia moja, na mji uliotoka wenye watu mia moja, utabakiziwa watu kumi, kwa nyumba ya Israeli. Maana BWANA awaambia hivi nyumba ya Israeli, Nitafuteni mimi, nanyi mtaishi; bali msitafute Betheli, wala msiingie Gilgali, wala msipite kwenda Beer-sheba; kwani Gilgali hakika yake itakwenda utumwani, na Betheli itakuwa ubatili. Mtafuteni BWANA, nanyi mtaishi; asije akawaka kama moto katika nyumba ya Yusufu, nao ukateketeza, asiwepo mtu awezaye kuuzima katika Betheli. Ninyi mnaogeuza hukumu kuwa uchungu, na kuiangusha haki chini, mtafuteni yeye afanyaye Kilimia na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA, ndilo jina lake; yeye aletaye uharibifu wa ghafla juu ya wenye nguvu, hata kuiharibu ngome.

Soma Amosi 5