Amosi 5:1-9
Amosi 5:1-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Sikilizeni maombolezo yangu juu yenu, enyi Waisraeli: Umeanguka na hutainuka tena ewe binti Israeli! Umeachwa pweke nchini mwako, hamna hata mtu wa kukuinua. Maana Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu 1,000 watatoka mjini kwenda kupigana lakini watarejea 100 tu; wataondoka watu 100 wa kijiji kimoja lakini watanusurika watu kumi tu.” Mwenyezi-Mungu awaambia hivi Waisraeli: “Nitafuteni mimi nanyi mtaishi! Lakini msinitafute huko Betheli wala msiende Gilgali wala msivuke kwenda Beer-sheba. Maana wakazi wa Gilgali, hakika watachukuliwa uhamishoni, na Betheli utaangamizwa!” Mtafuteni Mwenyezi-Mungu, nanyi mtaishi! La sivyo, atawalipukia wazawa wa Yosefu kama moto; moto utawateketeza wakazi wa Betheli na hakuna mtu atakayeweza kuuzima. Tahadhari enyi mnaogeuza haki kuwa uchungu, na kuuona uadilifu kuwa kama takataka! Huyo aliyezifanya Kilimia na sayari Orioni, ambaye huligeuza giza nene kuwa mchana, na mchana kuwa usiku; yeye ambaye ayaitaye pamoja maji ya bahari na kuyamwaga juu ya nchi kavu, Mwenyezi-Mungu ndilo jina lake. Yeye ndiye anayewaangamiza wenye nguvu, na kuziharibu ngome zao.
Amosi 5:1-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lisikieni neno hili nilitamkalo liwe maombolezo juu yenu, enyi nyumba ya Israeli. Bikira wa Israeli ameanguka; hatainuka tena; Ameangushwa katika nchi yake; hakuna mtu wa kumwinua. Kwa kuwa Bwana MUNGU asema hivi; Mji uliotoka nje wenye watu elfu moja, utabakiziwa watu mia moja, na mji uliotoka wenye watu mia moja, utabakiziwa watu kumi, kwa nyumba ya Israeli. Maana BWANA awaambia hivi nyumba ya Israeli, Nitafuteni mimi, nanyi mtaishi; bali msitafute Betheli, wala msiingie Gilgali, wala msipite kwenda Beer-sheba; kwani Gilgali hakika yake itakwenda utumwani, na Betheli itakuwa ubatili. Mtafuteni BWANA, nanyi mtaishi; asije akawaka kama moto katika nyumba ya Yusufu, nao ukateketeza, asiwepo mtu awezaye kuuzima katika Betheli. Ninyi mnaogeuza hukumu kuwa uchungu, na kuiangusha haki chini, mtafuteni yeye afanyaye Kilimia na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA, ndilo jina lake; yeye aletaye uharibifu wa ghafla juu ya wenye nguvu, hata kuiharibu ngome.
Amosi 5:1-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lisikieni neno hili nilitamkalo liwe maombolezo juu yenu, enyi nyumba ya Israeli. Bikira wa Israeli ameanguka; hatainuka tena; Ameangushwa katika nchi yake; hakuna mtu wa kumwinua. Kwa kuwa Bwana MUNGU asema hivi; Mji uliotoka nje wenye watu elfu, utasaziwa watu mia, na mji uliotoka wenye watu mia, utasaziwa watu kumi, kwa nyumba ya Israeli. Maana BWANA awaambia hivi nyumba ya Israeli, Nitafuteni mimi, nanyi mtaishi; bali msitafute Betheli, wala msiingie Gilgali, wala msipite kwenda Beer-sheba; kwani Gilgali hakika yake itakwenda utumwani, na Betheli itakuwa ubatili. Mtafuteni BWANA, nanyi mtaishi; asije akawaka kama moto katika nyumba ya Yusufu, nao ukateketeza, asiwepo mtu awezaye kuuzima katika Betheli. Ninyi mnaogeuza hukumu kuwa uchungu, na kuiangusha haki chini, mtafuteni yeye afanyaye Kilimia na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza kwa usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA, ndilo jina lake; yeye aletaye uharibifu wa ghafula juu yao walio hodari, hata uharibifu uipate ngome.
Amosi 5:1-9 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Sikia neno hili, ee nyumba ya Israeli, ombolezo hili ninalifanya kuwahusu ninyi: “Bikira Israeli ameanguka, kamwe hatainuka tena, ameachwa pweke katika nchi yake, hakuna yeyote wa kumwinua.” Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: “Wakati mmoja wa miji yako utakapopeleka watu elfu moja vitani kwa ajili ya Israeli, mia moja tu watarudi; wakati mji utakapopeleka mia moja, kumi tu ndio watarudi hai.” Hili ndilo BWANA asemalo kwa nyumba ya Israeli: “Nitafuteni mpate kuishi; msitafute Betheli, msiende Gilgali, msisafiri kwenda Beer-Sheba. Kwa maana kwa hakika Gilgali itakwenda uhamishoni, na Betheli itafanywa kuwa si kitu.” Mtafuteni BWANA mpate kuishi, au atafagia nyumba ya Yosefu kama moto; utawateketeza, nayo Betheli haitakuwa na yeyote wa kuuzima. Ninyi ambao mnageuza haki kuwa uchungu na kuiangusha haki chini (yeye ambaye alifanya Kilimia na Orioni, ambaye hugeuza giza kuwa mapambazuko na mchana kuwa usiku, ambaye huyaita maji ya bahari na kuyamwaga juu ya uso wa nchi: BWANA ndilo jina lake; yeye hufanya maangamizo kwenye ngome na kufanya mji uliozungushiwa ngome kuwa ukiwa)