Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezekieli 46

46
Kanuni nyinginezo
1 # Isa 66:23; Eze 45:17; Ebr 4:9,10 Bwana MUNGU asema hivi; Lango la ua wa ndani, lielekealo upande wa mashariki litafungwa siku sita za kazi; lakini siku ya sabato litafunguliwa, na siku ya mwezi mwandamo litafunguliwa. 2#Eze 44:3; Mt 25:10 Naye mkuu ataingia kwa njia ya ukumbi wa lango lile, upande wa nje, naye atasimama karibu na mwimo wa lango, nao makuhani wataitengeneza sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka zake za amani, naye ataabudu penye kizingiti cha lango; kisha atatoka; lakini lango lile halitafungwa hadi wakati wa jioni. 3#Zab 100:4; Lk 1:10 Watu wa nchi nao wataabudu mbele ya mlango wa lile lango mbele za BWANA, siku za sabato, na siku za mwezi mwandamo. 4#Hes 28:5,9,11,12; Eze 45:17 Nayo sadaka ya kuteketezwa, ambayo mkuu atamtolea BWANA siku ya sabato, itakuwa wana-kondoo sita wakamilifu, na kondoo dume mkamilifu. 5#Hes 28:12; Eze 45:24 Na sadaka ya unga itakuwa efa moja kwa kondoo dume, na sadaka ya unga kwa wale wana-kondoo, kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta kwa efa moja. 6Na siku ya mwezi mwandamo itakuwa ni ng'ombe dume mchanga mkamilifu; na wana-kondoo sita, na kondoo dume; nao watakuwa wakamilifu. 7Naye atatengeneza sadaka ya unga, efa moja kwa ng'ombe dume, na efa moja kwa kondoo dume, na kwa wale wana-kondoo, kwa kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta kwa efa moja. 8Naye mkuu atakapoingia, ataingia kwa njia ya ukumbi wa lango lile, naye atatoka kwa njia iyo hiyo. 9#Kut 23:14,17; Kum 16:16; Zab 84:7 Lakini watu wa nchi watakapokuja mbele za BWANA katika sikukuu zilizoamriwa, yeye aingiaye kwa njia ya lango la upande wa kaskazini ili kuabudu, atatoka kwa njia ya lango la upande wa kusini; na yeye aingiaye kwa njia ya lango la upande wa kusini, atatoka kwa njia ya lango la upande wa kaskazini; hatarudi kwa njia ya lango aliloingia kwalo, lakini atatoka kwa kwenda mbele moja kwa moja. 10Naye mkuu atakapoingia, ataingia katikati yao, nao, watakapotoka, watatoka wote pamoja. 11Na katika sikukuu hizo, na sikukuu nyingine zilizoamriwa, sadaka ya unga itakuwa efa moja kwa ng'ombe mmoja, na efa moja kwa kondoo dume mmoja, na kwa wale wana-kondoo kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta kwa efa moja. 12#Law 1:3; 23:37; Hes 29:39; Mt 20:28; Yn 10:18; Gal 2:20; Tit 2:14; Eze 44:3 Naye mkuu atakapotengeneza sadaka atoayo kwa hiari yake mwenyewe, sadaka ya kuteketezwa, au sadaka za amani, ziwe sadaka amtoleazo BWANA kwa hiari yake mwenyewe, mtu mmoja atamfungulia lango lile lielekealo upande wa mashariki, naye ataitoa sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka zake za amani, kama afanyavyo siku ya sabato; kisha atatoka; na baada ya kutoka kwake mtu mmoja atalifunga lango. 13#Kut 29:38; Hes 28:3 Nawe utamtoa mwana-kondoo wa mwaka mmoja, mkamilifu, kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA kila siku; kila siku asubuhi utamtoa. 14Nawe utaitoa sadaka ya unga pamoja nayo kila siku asubuhi, sehemu ya sita ya efa moja, na sehemu ya tatu ya hini moja ya mafuta; kuchanganya na unga ule mzuri; sadaka ya unga kwa BWANA daima, kwa amri ya milele. 15Hivyo ndivyo watakavyomtoa mwana-kondoo, na sadaka ya unga, na mafuta, kila siku asubuhi, kuwa sadaka ya kuteketezwa ya daima.
16Bwana MUNGU asema hivi; Mkuu akimpa mwanawe awaye yote zawadi, ni urithi wake, itakuwa mali ya wanawe; ni milki yao ya kurithiwa. 17#Law 25:9,10; Isa 61:2 Bali akimpa mmoja wa watumishi wake baadhi ya urithi wake, itakuwa mali yake mpaka mwaka wa kuacha huru; ndipo itakapomrudia mkuu; lakini urithi wake, huo utakuwa wa wanawe. 18#Zab 78:72; Yer 23:5,6; Eze 45:8 Tena mkuu hatawaondolea watu urithi wao, hata kuwatoa kwa nguvu katika milki yao; atawapa wanawe urithi katika mali yake mwenyewe, watu wangu wasije wakatawanyika, kila mtu mbali na milki yake.
19Ndipo akanileta kati ya maingilio, yaliyokuwa kando ya lango, mpaka katika vyumba vitakatifu vya makuhani, vilivyoelekea upande wa kaskazini; na tazama, palikuwa na mahali, upande wa nyuma ulioelekea magharibi. 20#2 Nya 35:13; Law 2:4-7; Eze 44:19,29; 43:23,24; Kut 19:10; Ebr 10:22 Akaniambia, Hapa ndipo mahali pa makuhani, watakapoitokosa sadaka ya hatia, na sadaka ya dhambi, watakapoioka sadaka ya unga; kusudi wasizilete nje katika ua wa nje, na kuwatakasa watu. 21Kisha akanileta mpaka ua wa nje, akanipitisha karibu na pembe nne za ua huo; na tazama, katika kila pembe ya ua huo palikuwa na kiwanja. 22Katika pembe nne za ua huo palikuwa na viwanja vilivyoungana, urefu wake dhiraa arubaini, na upana wake thelathini; viwanja hivyo vinne vya pembeni vilikuwa vya kipimo kimoja. 23Tena palikuwa na safu ndani yake pande zote, kuvizunguka vile viwanja vinne; tena palifanywa meko ya kutokosea, chini ya safu pande zote. 24#Rum 12:1; 15:16; Ebr 13:16 Ndipo akaniambia, Hizi ni nyumba za kutokosea, ambamo wahudumu wa nyumba watatokosa sadaka za watu.

Iliyochaguliwa sasa

Ezekieli 46: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia