Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezekieli 47

47
Maji yatokayo hekaluni
1 # Zek 13:1; 14:8; Yn 7:38; Ufu 22:1; Zab 46:4; Yoe 3:18 Baadaye akanileta tena mpaka lango la nyumba; na tazama, maji yalitoka chini ya kizingiti cha nyumba, kwa njia ya mashariki, maana upande wa mbele wa nyumba ulielekea upande wa mashariki; nayo maji yakashuka toka chini ya upande wa kulia wa nyumba, upande wa kusini wa madhabahu. 2Ndipo akanileta nje kwa njia ya lango upande wa kaskazini, akanizungusha kwa njia ya nje mpaka lango la nje, kwa njia yake iliyoelekea mashariki; na tazama, maji yalitoka upande wa kulia. 3#Eze 40:3; Zek 2:1; Ufu 11:1 Na alipotoka mtu yule, mwenye uzi wa kupimia mkononi mwake, akielekea mashariki, akapima dhiraa elfu moja, akanivusha maji yale; maji yakafika mpaka katika vifundo vya miguu. 4Kisha akapima dhiraa elfu moja, akanivusha maji yale, maji yakafika mpaka magoti. Kisha akapima dhiraa elfu moja, akanivusha, maji yakafika mpaka viuno. 5Kisha akapima dhiraa elfu moja, yakawa mto nisioweza kuuvuka; maana maji yamezidi, maji ya kuogelea, mto usiovukika.
6Akaniambia, Mwanadamu, je! Umeona haya? Kisha akanichukua akanirudisha mpaka ukingo wa mto. 7#Zab 1:3; 92:12; Isa 41:19; Ufu 22:2 Basi nikiisha kurudi, tazama, kando ya ukingo wa mto ilikuwapo miti mingi sana, upande huu na upande huu. 8#Zek 2:11; Mal 1:11; Ufu 17:15 Ndipo akaniambia, Maji haya yanatoka kwenda pande za nchi ya mashariki, nayo yanashuka mpaka Araba, na kuingia katika bahari;#47:8 Yaani, Bahari ya Chumvi. maji yatokezwayo yataingia baharini, na maji yake yatakuwa safi. 9#Yn 5:25; 6:63; 1 Kor 15:45 Tena itakuwa, kila kiumbe hai kisongamanacho, kila mahali itakapofika mito hiyo, kitaishi; kutakuwapo wingi mkubwa wa samaki, kwa sababu maji haya yamefika huko maana maji yale yatakuwa safi, na kila kitu kitaishi popote utakapofika mto huo. 10#Mt 4:19; Hes 34:6; Yos 23:4; Eze 47:15 Tena itakuwa, wavuvi watasimama karibu nao; toka Engedi mpaka En-eglaimu, patakuwa ni mahali pa kutandazia nyavu; samaki wao watakuwa namna zao mbalimbali, kama samaki wa bahari kubwa, wengi sana. 11Bali mahali penye matope, na maziwa yake, hayataponywa; yataachwa yawe ya chumvi. 12#Ayu 8:16; Zab 1:3; Isa 61:3; Ufu 22:2 Na karibu na mto, juu ya ukingo wake, upande huu na upande huu, utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayataisha kamwe; utatoa matunda mapya kila mwezi, kwa sababu maji yake yanatoka mahali patakatifu; na matunda yake yatakuwa ni chakula; na majani yake yatakuwa ni dawa.
Mipaka mipya ya nchi
13 # Mwa 48:5; 1 Nya 5:1; Yer 3:18; Eze 48:4,5 Bwana MUNGU asema hivi; Huu ndio mpaka ambao mtaigawanya nchi iwe urithi sawasawa na makabila kumi na mawili ya Israeli; kwa Yusufu, mafungu mawili. 14#Hes 34:2; Eze 48:29 Nanyi mtaimiliki, mtu huyu sawasawa na huyu; ambayo niliuinua mkono wangu kuwapa baba zenu; na nchi hii itawaangukia kuwa urithi. 15#Eze 48:1; Hes 34:8 Na huu ndio mpaka wa nchi; upande wa kaskazini, toka bahari kubwa, kwa njia ya Hethloni, mpaka maingilio ya Sedada; 16#2 Fal 14:25; Amo 6:2,14; 2 Sam 8:8 Hamathi, na Berotha, na Sibraimu, ulio katikati ya mpaka wa Dameski na mpaka wa Hamathi; na Haser-hatikoni, ulio karibu na mpaka wa Haurani. 17#Hes 34:9 Nao mpaka toka baharini utakuwa Hasar-enoni, penye mpaka wa Dameski, na kaskazini kuelekea upande wa kaskazini ndio mpaka wa Hamathi. Huu ndio upande wa kaskazini. 18Na upande wa mashariki, kati ya Haurani na Dameski, na Gileadi na nchi ya Israeli, utakuwa Mto Yordani; mtapima toka mpaka wa upande wa kaskazini hata bahari ya mashariki. Huu ndio upande wa mashariki. 19Na upande wa kusini, kuelekea kusini, utakuwa ni kutoka Tamari mpaka maji ya Meriba-Kadeshi, mpaka kijito cha Misri, mpaka bahari kubwa. Huu ndio upande wa kusini, kuelekea kusini. 20Na upande wa magharibi, utakuwa ni bahari kubwa, kutoka mpaka wa kusini mpaka mahali penye kuelekea maingilio ya Hamathi. Huu ndio upande wa magharibi. 21Basi ndivyo mtakavyojigawanyia nafsi zenu nchi hii, sawasawa na makabila ya Israeli. 22#Mdo 2:5; Efe 2:19-22; Rum 10:12 Tena itakuwa mtaigawanya kwa kura, kuwa urithi kwenu, na kwa wageni wakaao kwenu kama ugeni, watakaozaa watoto kati yenu, nao watakuwa kwenu, kama wazaliwa miongoni mwa wana wa Israeli; watakuwa na urithi pamoja nanyi kati ya makabila ya Israeli. 23Tena itakuwa, mgeni akaaye katika kabila iwayo yote, atapewa urithi katika kabila asema Bwana MUNGU.

Iliyochaguliwa sasa

Ezekieli 47: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia