Waraka kwa Waebrania 8
8
Mpatanishi wa Agano bora zaidi
1 #
Zab 110:1; Ebr 4:14 Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, 2mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu. 3Maana kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa. 4Kama angekuwa juu ya nchi, asingekuwa kuhani; maana wako watoao sadaka kama iagizavyo sheria; 5#Kut 25:40; Kol 2:17 watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule uliooneshwa katika mlima. 6#Ebr 7:22; 12:24; 2 Kor 3:6 Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora. 7Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili. 8#Yer 31:31-34; Ebr 10:16,17 Maana, anapowalaumu, asema,
Angalia, siku zinakuja, asema Bwana,
Nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya;
9 #
Kut 19:5,6 Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao,
Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri.
Kwa sababu hawakudumu katika agano langu,
Mimi nami sikuwajali asema Bwana.
10Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli
Baada ya siku zile, asema Bwana;
Nitawapa sheria zangu katika fikira zao,
Na katika mioyo yao nitaziandika;
Nami nitakuwa Mungu kwao,
Nao watakuwa watu wangu.
11Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake,
Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana;
Kwa maana wote watanijua,
Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.
12Kwa sababu nitawasamehe maovu yao,
Na dhambi zao sitazikumbuka tena.
13 #
Rum 10:4
Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa kiko karibu kutoweka.
Iliyochaguliwa sasa
Waraka kwa Waebrania 8: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.