Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 38

38
Kuugua kwa Hezekia
1 # 2 Fal 20:1; 2 Nya 32:24 Siku hizo Hezekia aliugua, akawa karibu kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, BWANA asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. 2Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba BWANA, 3#Neh 5:19 akasema, Ee BWANA, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia kwa uchungu. 4Ikawa, neno la BWANA likamjia Isaya, kusema, 5Nenda ukamwambie Hezekia, BWANA, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano. 6#Isa 37:35 Nami nitakuokoa wewe, na mji huu, kutoka kwa mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu. 7#2 Fal 20:8; Isa 37:30 Jambo hili liwe ishara kwako, itokayo kwa BWANA, ya kuwa BWANA atalitimiza jambo hili alilolisema; 8Tazama, nitakirudisha nyuma kivuli madaraja kumi, ambayo kilishuka juu ya duara ya Ahazi kwa sababu ya jua. Basi jua likarudi madaraja kumi katika hiyo duara, ambayo limekwisha kushuka.
9Haya ndiyo maandiko ya Hezekia, mfalme wa Yuda, alipokuwa mgonjwa, naye akapona ugonjwa wake.
10 # Zab 102:24 Nilisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu;
Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu.
11 # Ayu 35:14; Zab 27:13; 31:22; 116:9 Nilisema, Sitamwona BWANA, yeye BWANA, katika nchi ya walio hai;
Sitamwona mwanadamu tena pamoja na hao wakaao duniani.
12 # Ayu 7:6; 2 Kor 5:4; Zab 102:11,23,24 Makao yangu yameondolewa kabisa,
yamechukuliwa kama hema ya mchungaji;
Nimekunja maisha yangu kama mfumaji;
atanikatilia mbali na kitanda cha mfumi;
Tangu mchana hata usiku wanimaliza.
13Nilijituliza hata asubuhi;
kama simba, anaivunja mifupa yangu yote;
Tangu mchana hata usiku wanimaliza.
14 # Isa 59:11 Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia;
Niliomboleza kama hua;
macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu;
Ee BWANA, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu.
15 # Ayu 7:11 Niseme nini? Yeye amenena nami,
na yeye mwenyewe ametenda hayo;
Nitakwenda polepole miaka yangu yote,
kwa sababu ya uchungu wa nafsi yangu.
16Ee Bwana, kwa mambo hayo watu huishi;
Na uhai wa roho yangu u katika hayo yote;
Kwa hiyo uniponye na kunihuisha.
17Tazama; nilikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu;
Lakini kwa kunipenda umeniokoa kutoka kwa shimo la uharibifu;
Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.
18 # Zab 6:5; 30:9; Mhu 9:10 Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu;
mauti haiwezi kukuadhimisha;
Wale washukao shimoni hawawezi kuutumainia uaminifu wako.
19 # Kum 4:9; Zab 78:3 Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo;
Baba atawajulisha watoto uaminifu wako.
20 # Zab 9:13; 46:1; 66:12 BWANA yu tayari kunipa wokovu.
Basi, kwa vinubi tutaziimba nyimbo zangu,
Siku zote za maisha yetu nyumbani mwa BWANA.
21 # 2 Fal 20:7 Maana Isaya amesema, Na watwae mkate wa tini, wakauweke juu ya jipu, naye atapona. 22Tena Hezekia alikuwa amesema, Iko ishara gani ya kunionesha ya kuwa nitapanda niingie nyumbani mwa BWANA?

Iliyochaguliwa sasa

Isaya 38: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia