Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 39

39
Wajumbe kutoka Babeli wakaribishwa
1 # 2 Fal 20:12 Wakati huo Merodak-baladani, mwana wa Baladani, mfalme wa Babeli, alipeleka barua na zawadi kwa Hezekia; kwa maana amepata habari kwamba amekuwa mgonjwa, na kwamba amepona. 2#2 Nya 32:31 Hezekia akawafurahia, akawaonesha nyumba yake yenye vitu vyake vya thamani, fedha na dhahabu, na manukato, na marhamu ya thamani, na nyumba yote yenye silaha zake za vita, na vitu vyote vilivyoonekana katika hazina zake; hapakuwa na kitu nyumbani mwake wala katika ufalme wake ambacho hakuwaonesha. 3Ndipo Isaya nabii akamwendea mfalme Hezekia, akamwambia, Watu hawa walisema nini? Nao wametoka wapi kuja kwako? Hezekia akasema, Wametoka katika nchi iliyo mbali, wakaja kwangu toka Babeli. 4Ndipo akasema, Wameona nini katika nyumba yako? Hezekia akajibu, Wameviona vitu vyote vilivyomo nyumbani mwangu; hapana kitu katika hazina zangu ambacho sikuwaonesha. 5Ndipo Isaya akamwambia Hezekia, Basi, lisikie neno la BWANA wa majeshi. 6#Law 26:33; Kum 28:64; 1 Fal 14:15; 2 Nya 36:18; Amo 5:27 Tazama, siku zinakuja, ambazo vitu vyote vilivyomo nyumbani mwako, na hivyo vilivyowekwa akiba na baba zako hata leo, vitachukuliwa mpaka Babeli; hapana kitu chochote kitakachosalia; asema BWANA. 7#Dan 1:1-7; 2 Fal 24:10-16; 2 Nya 36:10 Na baadhi ya wana wako utakaowazaa, watakaotoka kwako, watawachukulia mbali; nao watakuwa matowashi katika jumba la mfalme wa Babeli. 8#1 Sam 3:18 Ndipo Hezekia akamwambia Isaya, Neno la BWANA ulilolinena ni jema. Tena akamwambia, Maana alifikiri, kutakuwapo na amani na usalama katika siku zangu mimi.

Iliyochaguliwa sasa

Isaya 39: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia