Yakobo 2:2-4
Yakobo 2:2-4 SRUV
Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Wewe keti hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Wewe simama pale, au keti miguuni pangu, je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo maovu?