Waamuzi 6
6
Ukandamizaji wa Wamidiani
1 #
Law 26:14; Amu 2:19; Mwa 25:2; Hes 25:17; Hab 3:7 Kisha wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu mbele za macho ya BWANA; BWANA akawatia mikononi mwa Midiani muda wa miaka saba 2#1 Sam 13:6; Ebr 11:38 Mkono wa Midiani ulikuwa na nguvu juu ya Israeli; tena kwa sababu ya Midiani wana wa Israeli walijifanyia hayo mashimo yaliyo milimani, na hayo mapango, na hizo ngome. 3#Mwa 29:1; Amu 7:12; 8:10; 1 Fal 4:30; Ayu 1:3 Basi ikawa, hapo Israeli walipokuwa wamepanda mashamba, Wamidiani wakakwea, na Waamaleki, na hao wana wa mashariki; wakawavamia; 4#Law 26:16; Kum 28:30; Ayu 31:7,8; Yer 5:17; 12:12,13; Mik 6:15 wakapiga kambi juu yao, na kuyaharibu hayo mavuno ya nchi, hadi kufika Gaza, wala hawakuacha katika Israeli riziki zozote; kondoo, wala ng'ombe, wala punda. 5Kwa maana walikwea na ng'ombe zao na hema zao, wakaja mfano wa nzige kwa wingi; wao na ngamia zao pia walikuwa hawana hesabu; nao waliingia katika hiyo nchi ili kuiharibu. 6#Zab 50:15; 78:34; Hos 5:15 Israeli walitwezwa sana kwa sababu ya Wamidiani; nao wana wa Israeli wakamlilia BWANA.
7Kisha ikawa, hapo wana wa Israeli walipomlilia BWANA kwa sababu ya Midiani, 8BWANA akamtuma nabii aende kwa hao wana wa Israeli; naye akawaambia, BWANA, yeye Mungu wa Israeli, asema hivi, Mimi niliwaleta ninyi mkwee kutoka Misri, nikawatoa katika nyumba ya utumwa; 9nami niliwaokoa na mikono ya Wamisri, na mikono ya wote waliokuwa wakiwaonea, nami niliwafukuza watoke mbele zenu, nami niliwapa ninyi nchi yao; 10#2 Fal 17:35; Yer 10:2 kisha niliwaambia, Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu; msiiche miungu ya Waamori, ambayo mnakaa katika nchi yao; lakini hamkuitii sauti yangu.
Gideoni aitwa na Mungu
11 #
Yos 17:2; Amu 8:2 Malaika wa BWANA akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwaabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani. 12#Mwa 16:7-13; Amu 13:3; Lk 1:11,28 Malaika wa BWANA akamtokea, akamwambia, BWANA yuko pamoja nawe, Ee shujaa. 13#Zab 89:49; Isa 59:1; 2 Nya 15:2 Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa BWANA yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye BWANA, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani. 14#1 Sam 12:11; Ebr 11:32; Yos 1:9 BWANA akamtazama, akasema, Nenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma? 15#1 Sam 9:21 Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu. 16#Kut 3:12; Yos 1:5 BWANA akamwambia, Hakika nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kama mtu mmoja. 17#Kut 4:1 Naye akamwambia, Kama nimepata kibali mbele za macho yako, basi unioneshe ishara, ya kuwa ndiwe wewe unayesema nami. 18#Mwa 18:3 Tafadhali, usiondoke hapa hadi nikujie, nikatoe zawadi yangu, na kuiweka mbele zako. Akasema, Nitangoja hadi utakaporudi. 19Basi Gideoni akaingia ndani, akaandaa mwana-mbuzi, na mikate isiyotiwa chachu, ya efa ya unga; akaitia ile nyama katika kikapu, akautia mchuzi katika nyungu, akamletea hapo nje chini ya mwaloni, akampa. 20#Amu 13:19; 1 Fal 18:33 Naye malaika wa Mungu akamwambia, Itwae nyama na mikate isiyotiwa chachu, uiweke juu ya mwamba huu, ukaumwage huu mchuzi. Akafanya hivyo. 21#Law 9:24; 2 Nya 7:1 Ndipo malaika wa BWANA akanyosha ncha ya fimbo ile iliyokuwa mkononi mwake, akaigusa ile nyama na ile mikate; moto ukatoka mwambani, ukaiteketeza ile nyama na mikate; malaika wa BWANA akaondoka mbele ya macho yake.
22 #
Mwa 16:13; 32:30; Kut 33:20; Amu 13:22 Gideoni akaona ya kuwa ni malaika wa BWANA; Gideoni akasema, Ole wangu, Ee Bwana MUNGU! Kwa kuwa nimemwona BWANA uso kwa uso. 23#Dan 10:19; Lk 24:36 BWANA akamwambia “Amani iwe pamoja nawe; usiogope; hutakufa”. 24#Mwa 22:14; Kut 17:15; Yer 33:16; Eze 48:35; Amu 8:32 Ndipo Gideoni akamjengea BWANA madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu;#6:24 Yehova-shalomu: maana yake ni, BWANA ni Amani. hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri.
25 #
Kut 34:13; Kum 7:5; Amu 3:7 Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera#6:25 yaani ile miimo ya kuabudia Baali. ile iliyo karibu nayo; 26ukamjengee BWANA, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata.
Gideoni abomoa madhabahu ya Baali
27 #
Yn 3:1
Ndipo Gideoni akatwaa watu kumi miongoni mwa watumishi wake, akafanya kama BWANA alivyomwambia; lakini kwa kuwa aliwaogopa watu wa nyumba ya baba yake, na watu wa mji, hakuweza kuyatenda hayo wakati wa mchana, basi aliyatenda usiku. 28Hata wakazi wa mji walipoamka asubuhi na mapema, wakaona madhabahu ya Baali imebomolewa, na ile Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na yule ng'ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya ile madhabahu iliyojengwa. 29Wakaambiana, Ni nani aliyetenda jambo hili? Walipotafuta habari na kuuliza, wakasema, Gideoni, mwana wa Yoashi, ndiye aliyetenda jambo hili. 30#Yn 16:2; Mdo 26:9 Ndipo wakazi wa mji wakamwambia Yoashi, Mlete mwanao, afe; kwa sababu ameibomoa madhabahu ya Baali na kwa sababu ameikata ile Ashera iliyokuwa karibu nayo. 31Yoashi akawaambia watu wote waliokuwa wakishindana naye, Je! Mtamtetea Baali? Au mtamwokoa ninyi? Yeye atakayemtetea na auawe kabla ya mapambazuko; kama yeye ni Mungu, na ajitetee nafsi yake, kwa sababu mtu mmoja ameibomoa madhabahu yake. 32Basi Yoashi akamwita Gideoni, Yerubaali siku hiyo, akisema, Baali na atete naye kwa ajili ya nafsi yake, kwa sababu ameibomoa madhabahu yake.
33 #
Yos 17:16; 19:18; 1 Fal 18:45; 21:23 Wakati huo Wamidiani na Waamaleki, na hao wana wa mashariki walikutana pamoja; wakavuka na kupanga hema zao katika bonde la Yezreeli. 34#Amu 3:10; 11:29; 13:25; 14:6,19; 1 Nya 12:18; 2 Nya 24:20; 1 Kor 12:8-11; Hes 10:3; Amu 3:27 Lakini Roho ya BWANA ikamjia juu yake Gideoni; naye akapiga tarumbeta; na Abiezeri walikutanika na kumfuata. 35Kisha akatuma wajumbe waende kati ya Manase yote; wao nao walikutana pamoja ili kumfuata; kisha akatuma wajumbe waende kwa Asheri, na kwa Zabuloni, na kwa Naftali; nao wakakwea ili kumlaki.
Ishara ya ngozi ya kondoo
36Gideoni akamwambia Mungu, Ikiwa wewe utawaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema, 37#Kut 4:3-7; Kum 32:2; Zab 72:6; Hos 6:3,4; 14:5 Tazama, nitaweka ngozi ya kondoo katika kiwanja cha kupuria; na kama ukiwapo umande juu ya ngozi tu, na nchi yote ikiwa kavu, basi, hapo ndipo nitakapojua ya kuwa utawaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema. 38Ikawa hivyo; kwa maana aliondoka asubuhi na mapema, akaikamua ile ngozi, akautoa ule umande katika ile ngozi, bakuli zima la maji. 39#Mwa 18:32 Gideoni akamwambia Mungu, Hasira yako isiwake juu yangu, nami nitasema mara hii tu; nakuomba, nijaribu kwa ngozi hii mara hii tu; sasa ngozi tu na iwe kavu, na uwe umande juu ya nchi yote. 40Mungu akafanya hivyo usiku ule; maana ile ngozi tu ilikuwa kavu, napo palikuwa na umande juu ya nchi yote.
Iliyochaguliwa sasa
Waamuzi 6: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.