Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 139:13-24

Zaburi 139:13-24 SRUV

Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu. Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa njia ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana, Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi katika pande za chini za nchi; Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Kitabuni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado. Mawazo yako ni mazito sana kwangu; Ee Mungu; nayo ni makuu sana. Kama ningeyahesabu ni mengi kuliko mchanga; Niamkapo ningali pamoja nawe. Ee Mungu, laiti ungewaua waovu! Na laiti watu wa damu wangetoka kwangu; Wale wanaokusema kwa ubaya, na kutenda maovu juu ya jina lako bure. Je! BWANA nisiwachukie wanaokuchukia? Nisiudhike nao watu wanaokuasi? Nawachukia kwa upepo wa chuki, Wamekuwa adui kwangu. Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu; Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele.

Soma Zaburi 139