Zaburi 45:9-17
Zaburi 45:9-17 SRUV
Binti za wafalme wamo Miongoni mwa akina bibi wako wastahiki. Katika mkono wako wa kulia amesimama malkia Akiwa amevaa dhahabu safi ya Ofiri. Sikia, binti, utazame, utege sikio lako, Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako. Naye mfalme atautamani uzuri wako, Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie. Na watu wa Tiro wanakushawishi kwa zawadi, Nao matajiri wa watu watajipendekeza kwako. Binti mfalme yumo ndani ana fahari tupu, Mavazi yake ni ya nyuzi za dhahabu. Anapelekwa kwa mfalme Na mavazi yaliyofumwa kwa uzuri. Wanawali wenzake wanaomfuata, Pia watapelekwa kwako. Watapelekwa kwa furaha na shangwe, Na kuingia katika nyumba ya mfalme. Badala ya baba zako watakuwapo watoto wako, Utawafanya kuwa wakuu katika nchi zote. Jina lako nitalifanya kuwa kumbukumbu Katika vizazi vyote. Kwa hiyo mataifa watakushukuru Milele na milele.