Zaburi 66
66
Sifa kwa ajili ya wema wa Mungu kwa Israeli
Kwa mwimbishaji. Wimbo. Zaburi.
1Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote,
2Imbeni utukufu wa jina lake,
Tukuzeni sifa zake.
3 #
Zab 18:44
Mwambieni Mungu, Matendo yako yatisha kama nini!
Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako,
Adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako.
4 #
Zab 67:3
Nchi yote itakusujudia na kukuimbia,
Naam, italiimbia jina lako.
5 #
Zab 46:8
Njoni myaone matendo ya Mungu;
Hutisha kwa mambo awatendayo wanadamu;
6 #
Kut 14:21; Yos 3:14-17; Zab 78:13; Isa 63:13,14 Aligeuza bahari ikawa nchi kavu;
Katika mto walivuka kwa miguu;
Huko ndiko tulikomfurahia yeye.
7 #
Zab 11:4
Atawalaye kwa uweza wake milele;
Ambaye macho yake yanaangalia mataifa;
Hebu wanaoasi wasijitukuze nafsi zao.
8Enyi mataifa, mtukuzeni Mungu wetu,
Itangazeni sauti ya sifa zake;
9Aliyeiweka nafsi yetu katika uhai,
Wala hakuuacha mguu wetu usogezwe.
10 #
Zek 13:9
Kwa maana umetupima, Ee Mungu,
Umetujaribu inavyojaribiwa fedha.
11Ulituingiza ndani ya wavu,
Na kuweka viunoni mwetu mzigo uliotulemea.
12Uliwapandisha watu
Juu ya vichwa vyetu.
Tulipitia motoni na majini;
Ukatutoa na kutuleta kwenye ufanisi.
13 #
Zab 116:14,18; Mhu 5:4; Yon 2:9 Nitaingia nyumbani mwako na kafara;
Nitaondoa kwako nadhiri zangu;
14Ambazo midomo yangu ilizinena;
Kinywa changu kikazisema nilipokuwa taabuni.
15Kafara za vinono nitakutolea,
Pamoja na fukizo la kondoo dume,
Nitatoa ng'ombe pamoja na mbuzi.
16Njoni, sikieni, ninyi nyote mnaomcha Mungu,
Nami nitayatangaza aliyonitendea roho yangu.
17Nilimwita kwa kinywa changu,
Na sifa kuu zilikuwa chini ya ulimi wangu.
18 #
Ayu 11:14,15; Mit 15:29; Isa 1:15 Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu,
Bwana asingesikia.
19Hakika Mungu amesikia;
Ameisikiliza sauti ya maombi yangu.
20Na ahimidiwe Mungu asiyeyakataa maombi yangu,
Wala kuniondolea fadhili zake.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 66: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.