Zaburi 95
95
Mwito wa kuabudu na kutii
1Njoni, tumwimbie BWANA,
Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.
2Tuje mbele zake kwa shukrani,
Tumfanyie shangwe kwa zaburi.
3Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu,
Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.
4Mkononi mwake zimo bonde za dunia,
Hata vilele vya milima ni vyake.
5Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya,
Na mikono yake iliumba nchi kavu.
6 #
1 Fal 8:54; 1 Nya 6:13; Ezr 9:5; Dan 6:10; Lk 22:41; Mdo 7:60; 1 Kor 6:20; Efe 3:14; Ayu 35:10; Isa 54:5; Yn 1:3 Njoni, tuabudu, tusujudu,
Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.
7 #
Ebr 3:7-11,15; 4:7; Zab 95:7-11; Hes 14:22 Kwa maana ndiye Mungu wetu,
Na sisi tu watu wa malisho yake,
Na kondoo za mkono wake.
Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!
8 #
Kut 17:1-7; Hes 20:2-13 Msifanye mioyo yenu kuwa migumu;
Kama ilivyokuwa huko Meriba
Kama siku ile katika Masa jangwani.
9Hapo waliponijaribu baba zenu,
Wakanipima, wakayaona matendo yangu.
10 #
Ebr 3:10
Miaka arubaini nilichukizwa na kizazi kile,
Nikasema, Hawa ni watu wenye mioyo inayopotoka,
Na wanaopuuza njia zangu.
11 #
Hes 14:20-23; Kum 1:34-36; 12:9-10; Ebr 4:3,5 Ndipo Nikaapa kwa hasira yangu
Hawataingia katika pumziko langu.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 95: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.