Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Marko 8

8
Yesu Awalisha Watu Zaidi ya 4,000
(Mt 15:32-39)
1Wakati mwingine katika siku zile kundi kubwa la watu lilikusanyika na halikuwa na chakula. Yesu akawaita wanafunzi wake na kuwaambia, 2“Nawahurumia watu hawa, kwa sababu hata sasa wamekuwa nami kwa siku tatu, na hawana kitu cha kula.”
3Nikiwaacha waende majumbani mwao wakiwa na njaa, wataanguka njiani; na baadhi yao wametoka mbali.
4Wanafunzi wake wakamjibu, “Wapi mtu yeyote atapata chakula cha kutosha mahali hapa jangwani cha kuwalisha watu hawa?”
5Yesu akawauliza, “Mnayo mikate mingapi?” Wakajibu, “Saba.”
6Kisha Yesu akaliagiza kundi la watu kuketi chini ardhini Akachukua mikate ile saba, akashukuru, akaimega na kuwapa wanafunzi wake waigawe. Nao wakaigawa kwenye kundi. 7Kulikuwapo pia samaki wadogo wachache. Yesu akawabariki wale samaki na kuwaambia waigawe nayo pia.
8Watu walikula na kushiba. Wakakusanya vikapu saba vilivyojaa mabaki. 9Ilikuwa kama watu 4,000. Kisha Yesu akawaacha waende. 10Mara Yesu akapanda katika mashua na wanafunzi wake, na akafika katika wilaya ya Dalmanutha.
Baadhi ya Watu Wawa na Mashaka na Mamlaka ya Yesu
(Mt 16:1-4; Lk 11:16,29)
11Mafarisayo wakamwendea Yesu na kuanza kubishana naye. Ili kumjaribu wakamwomba ishara kutoka mbinguni. 12Yesu alihema kwa nguvu na kusema, “Kwa nini kizazi kinataka ishara? Ninawaambia ukweli: hakuna ishara itakayooneshwa kwa kizazi hiki.” 13Kisha Yesu akawaacha, akapanda tena katika mashua, na akaondoka kwenda upande wa pili wa ziwa.
Wafuasi Washindwa Kumwelewa Yesu
(Mt 16:5-12)
14Wakati huo huo wanafunzi walikuwa wamesahau kuleta mikate yoyote, na hawakuwa na kitu kingine isipokuwa mkate mmoja. 15Yesu akawaonya, akasema, “Muwe mwangalifu! Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na ile ya Herode.”
16Nao wakaanza kujadiliana haya miongoni mwao: “Labda alisema hivi kwa sababu hatukuwa na mkate wowote.”
17Akijua walichokuwa wakikisema, akawaambia, “Kwa nini mnajadiliana juu ya kutopata mkate? Je! Bado hamwoni na kuelewa? Je! Mmezifunga akili zenu. 18Mnayo macho; Je! Hamwoni? Mnayo masikio; Je! Hamwezi kusikia? Mnakumbuka? 19Nilipomega na kugawa mikate mitano kwa watu 5,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa masalia ya mikate?”
Wakasema “Kumi na viwili”.
20“Nilipomega na kugawa mikate saba kwa watu 4,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa masalia ya mikate?”
Wakasema “Saba”.
21Kisha akawaambia, “Bado hamwelewi?”
Yesu Amponya Kipofu katika Kijiji cha Bethsaida
22Walipofika katika kijiji cha Bethsaida, baadhi ya watu walimleta asiyeona kwa Yesu, na kumsihi Yesu amguse. 23Yesu alimshika mkono yule asiyeona na kumtoa nje ya kijiji. Kisha Yesu alimtemea mate yule asiyeona kwenye macho yake, akaweka mkono wake juu ya asiyeona, na kumwuliza, “Je! Unaona kitu chochote?”
24Kipofu akatazama juu na kusema, “Ninaona watu; wanaonekana kama miti inayotembea.”
25Kisha Yesu akaweka mikono yake tena kwenye macho ya yule asiyeona. Naye akafumbua wazi macho yake yote. Kwani alipona kutokuona kwake na kuona kila kitu kwa uwazi. 26Kisha Yesu akamwambia arudi nyumbani, na pia akamwambia, “Usiingie kijijini.”
Petro Atambua Yesu ni Nani
(Mt 16:13-20; Lk 9:18-21)
27Yesu na wanafunzi wake walikwenda kwenye vijiji vinavyozunguka Kaisaria Filipi. Wakiwa njiani aliwauliza wanafunzi wake, “Watu wanasema mimi ni nani?”
28Nao wakamjibu, “Yohana Mbatizaji. Wengine husema wewe ni Eliya. Na wengine husema wewe ni mmoja wa manabii.”
29Kisha akawauliza wao, “Na ninyi; Je! Mnasema mimi ni nani?”
Petro akamjibu, “Wewe ni masihi.”
30Kisha Yesu akawaonya wasimwambie mtu yeyote kuhusu yeye.
Yesu Asema ni Lazima Afe
(Mt 16:21-28; Lk 9:22-27)
31Ndipo alianza kuwafundisha akisema: “Mwana wa Adamu lazima apate mateso mengi, na kukatataliwa na wazee, wakuu wa makuhani na walimu wa Sheria, na ni lazima atauawa na Kufufufuka baada ya siku ya tatu.” 32Yesu aliwaambia haya kwa uwazi bila kuwaficha.
Baada ya mafundisho haya Petro alimchukua Yesu pembeni na kuanza kumkemea. 33Lakini Yesu aligeuka nyuma na kuwaangalia wanafunzi wake, na kumkemea Petro kwa kumwambia, “Shetani,#8:33 Shetani Jina la Mwovu lenye maana “Adui”. Maana ya Yesu ni kuwa Petro alikuwa akiongea kama Shetani. toka mbele yangu! Huyajali yale anayoyajali Mungu bali yale wanayoyaona wanadamu kuwa ni muhimu.”
34Kisha Yesu akaliita kundi lote pamoja na wanafunzi wake kwake, akawaambia, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, lazima ajikane yeye mwenyewe, na ni lazima auchukue msalaba wake mwenyewe kisha anifuate. 35Kwa kuwa kila anayetaka kuusalimisha uhai wake, ataupoteza, na yeyote atakayeupoteza uhai wake kwa ajili yangu na kwa ajili ya injili atausalimisha. 36Itampa mtu manufaa gani akiupata ulimwengu wote kisha akaupoteza uhai wake? 37Mtu anaweza kuubadilisha uhai wake na kitu gani? 38Hiki ni kizazi chenye dhambi na kisichokuwa na uaminifu. Hivyo, mtu yeyote atakayenionea haya mimi na mafundisho yangu, Mwana wa Adamu naye atamwonea haya mtu huyo siku ile atakaporudi katika utukufu wa Baba yake akiwa na malaika wake watakatifu.”

Iliyochaguliwa sasa

Marko 8: TKU

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia