Matendo 12
12
1PANAPO majira yaleytile Herode mfalme tw akanyosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa Kanisa. 2Akamwua Yakobo ndugu wa Yohana kwa upauga. 3Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamtwaa na Petro. Siku hizo ndizo siku za mikate isiyochachwa. 4Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa askari wanewane, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa mbele ya watu. 5Bassi Petro akalindwa gerezani, sala zikawa zinafanyika kwa juhudi sana na Kanisa mbele za Mungu kwa ajili yake. 6Hatta wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku uleule. Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili: walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza. 7Marra malaika wa Bwana akasimama karibu nae, nuru ikamulika chumbani mle, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo ikamwanguka. 8Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu: akafanya hivyo. Akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate. 9Akatoka, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni khabari ya kweli iliyofanyika na malaika; bali alidhani anaona njozi. 10Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hatta mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia. Wakatoka, wakapita katika njia moja; marra malaika akamwacha. 11Hatta Petro alipofahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na kutazamia kwa taifa la Wayahudi. 12Na alipokuwa akifikiri haya akafika nyumbani kwa Mariamu, mama yake Yohana, ambae jina lake la pili ni Marko; na wafu wengi wamekutana wakiomba. 13Na Petro alipobisha kilango cha lango, kijakazi, jina lake Rhoda, akaja kusikiliza. 14Alipoitambua sauti ya Petro, hakulifungua lango kwa furaha, bali alipiga mbio, akaingia ndani akawaambia kwamba Petro anasimama mbele ya lango. 15Wakamwambia, Una wazimu. Lakini yeye akakaza sana, akasema ya kwamba ndivyo bivyo. 16Wakanena, Ni malaika wake. Petro akafuliza kugonga; hatta walipokwislia kumfungulia wakamwona, wakastaajabu. 17Nae akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Enendeni, mkampashe Yakobo na ndugu zetu khabari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine. 18Hatta kulipopambazuka askari wakaingiwa na fadhaa nyingi, amekuwaje Petro. 19Na Herode alipomtafuta, asimwone, akawauliza walinzi, akaamuru wanawe. Nae akatelemka kutoka Yahudi kwenda Kaisaria, akakaa huko.
20Nae Herode aliwakasirikia sana watu wa Tʼuro na Sidon: wakamwendea kwa nia moja, na wakiislia kufanya urafiki na Blasto, mwenye kukitunza chumba cha mfalme cha kulalia, wakataka amani; kwa maana inchi yao ilipata riziki kwa inchi ya mfalme. 21Bassi siku moja iliyoazimiwa, Herode akajivika mavazi ya kifaume, akaketi katika kiti cha enzi, akatoa khotuba. 22Watu wakapiga kelele, wakinena, Ni sauti ya Mungu, si sauti ya mwana Adamu. 23Marra malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu: akaliwa na funza, akatoa roho.
24Neno la Bwana likazidi na kuenea. 25Na Barnaba na Saul, walipokwisha kuitimiza khuduma yao, wakarejea kutoka Yerusalemi wakamchukua pamoja nao Yohana aitwae Marko.
Iliyochaguliwa sasa
Matendo 12: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.