Matendo 13
13
1NA huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, Barnaba na Sumeon aitwae Niger, na Lukio Mkurene, na Manaen aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa Herode mfalme, na Saul. 2Bassi hawa walipokuwa wakimkhudumia Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Niwekeeni Barnaba na Saul kwa kazi ile niliyowaitia. 3Ndipo, wakiisha kuomba na kufunga, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.
4Bassi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Selukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hatta Kupro. 5Na walipokuwa katika Salamini wakalikhubiri neno la Bwana katika masunagogi ya Wayahudi, nao walikuwa nae Yohana kuwakhudumia. 6Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote cha Kupro, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa nwongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu: 7mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paolo, mtu mwenye akili. Yeye akawaita Barnaba na Saul waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. 8Lakini Eluma, yule mchawi (maana ndio tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha Imani. 9Lakini Saul ambae ndiye Paolo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, akanena, 10Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa shetani, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? 11Bassi, angalia, mkono wa Bwana ni juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda kitambo. Marra kiwi kikamwangukia na giza, akazungukazunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza. 12Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.
13Kiisha Paolo na wenziwe wakangʼoa nanga wakasafiri kutoka Pafo, wakafika Perga katika Pamfulia. Yohana akawaacha akarejea Yerusalemi. 14Lakini wao wakatoka Perga, wakapita kati ya inchi, wakafika Antiokia mji wa Pisidia, wakaingia katika sunagogi siku ya sabato, wakaketi. 15Kiisha baada ya kusomwa torati na chuo cha manabii, wakuu wa sunagogi wakatuma mtu kwao, na kuwaambia, Ndugu, kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa, lisemeni. 16Paolo akasimama, akawtipungia mkono, akanena, Enyi wanme wa Israeli, na ninyi mnaomcha Mungu, sikilizeni. 17Mungu wa watu hawa Israeli aliwachagua baba zetu, akawatukuza watu, walipokuwa wakikaa kama wageni katika inchi ya Misri, na kwa mkono ulioinuliwa akawatoa, akawaongoza. 18Na panapo muda wa miaka arubaini akawaruzuku katika jangwa. 19Na alipokwisha kuwaharibu mataifa saba katika inchi ya Kanaan akawajia inchi yao iwe urithi. 20Baada ya muda wa miaka aruba mia na khamsini, akawapa waamuzi hatta zamani za nabii Samwil. 21Khatimae wakaomba kupewa mfalme; Mungu akawapa Saul mwana wa Kish, mtu wa kabila ya Benjamin, kwa muda wa miaka arubaini. 22Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwmua Daud awe mfalme wao, akamshuhudia, akisema, Nimemwona Daud, mwana wa Yese, mtu nimpendae, atakaefanya mapenzi yangu vote. 23Katika uzao wake mtu huyo Mungu amewaletea Israeli Mwokozi, yaani Yesu, kama alivyoahidi, 24Yohana alipokuwa amekwisha kuwakhubiri watu wote wa Israeli khabari za ubatizo wa toba, kabla ya kuja kwake. 25Nae Yohana alipokuwa akimaliza mwendo wake alinena, Mwanidhani mimi kuwa nani? Mimi siye. Lakini, angalieni, anakuja mmoja nyuma yangu ambae mimi sistahili kumlegezea viatu vya miguu yake.
26Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, nao miongoni mwenu mnaomcha Mungu, kwenu ninyi neno la wokofu huu limepelekwa. 27Kwa maana wakaao Yerusalemi, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua huyu, wala sauti za manabii wanaosomwa killa sabato, wamezitimiza kwa kumhukumu. 28Na wasipopata sababu ya kumfisha wakamwomba Pilato auawe. 29Hatta walipomaliza yote aliyoandikiwa, wakamshusha katika mti, wakamweka kaburini. 30Lakini Mungu akamfufua: 31akaonwa siku nyingi nao waliopanda nae kutoka Galilaya hatta Yerusalemi, na hao ndio walio sasa mashahidi wake mbele va watu. 32Na sisi tunawakhubirieni ahadi ile waliyopewa baba zetu, ya kwamba Mungu ametutimizia sisi watoto wao ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu: 33kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili, Wewe ndiwe Mwana wangu, mimi leo nimekuzaa. 34Tena ya kuwa alimfufua, asipate kurudia uharibifu, amenena hivi, Nitakupa wewe mambo matakatifu ya Daud yaliyo amini. 35Kwa hiyo na penginepo anena, Hutamwachia Mtakatifu wako kuona uharibifu. 36Kwa maana Daud, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu. 37Bali huyu aliyefufuliwa na Mungu hakuona uharibifu. 38Bassi, ibainike kwenu, ndugu, ya kuwa kwa huyu mnakhubiriwa ondoleo la dhambi; 39na kwa huyu killa amwaminiye huhesabiwa kuwa hana khatiya katika mambo yale asiyoweza kuhesabiwa kuwa hana khatiya kwa torati ya Musa. 40Angalieni, bassi, isije khabari ile iliyonenwa katika manabii, 41Tazameni, enyi mnaodharau, kjitaajabuni, katowekeni; kwa kuwa natenda kazi mimi siku zenu, kazi msiyoisadiki kabisa, ijapo mtu akiwasimulia sana.
42Na walipokuwa wakitoka katika sunagogi la Wayahudi, watu wa mataifa wakawasihi kuwaambia maneno haya sabato ya pili. 43Sunagogi lilipofumukana, Wayahudi wengi na waongofu watawa wakashikamana na Paolo na Barnaba; nao, wakisema nao, wakawatia moyo kudumu katika neema ya Mungu.
44Hatta sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu. 45Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayabisha maneno yaliyonenwa na Paolo, wakibisha na kutukana. 46Paolo na Barnaba wakanena kwa uthabiti wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza: illakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, wala hamjioni nafsi zenu kuwa mmestahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia mataifa. 47Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana,
Nimekuweka uwe nuru ya mataifa,
Upate kuwa wokofu hatta mwisho wa dunia:
48Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini. 49Neno la Bwana likaenea katika inchi ile yote. 50Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watawa na watu wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paolo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao. 51Nao wakawakungʼutia mavumbi ya miguu yao, wakaenda Ikonio. 52Na wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu.
Iliyochaguliwa sasa
Matendo 13: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.