Matendo 3
3
1BASSI Petro na Yohana walikuwa wakipanda pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tissa. 2Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mama yake alichukuliwa na watu, wakamweka killa siku katika mlango wa hekalu nitwao Mzuri, illi aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu. 3Mtu huyu akiwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka. 4Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi. 5Akawaangalia, akitaraja kupewa kitu nao. 6Petro akanena, Fedha sina, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Mnazareti, simama uende. 7Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, marra nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikapata nguvu. 8Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda: akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka, akimsifu Mungu. 9Watu wote wakamwona akieuda, akimsifu Mungu. 10Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa ameketi na kuomba sadaka penye mlango mzuri wa hekalu: wakajaa ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata.
11Bassi yule kiwete aliyeponywa alipokuwa akiwashika Petro na Yohana, watu wote wakawakusanyikia mbio katika tao lile lililokwitwa tao la Sulemani; wakishangaa sana. 12Hatta Petro alipoona haya akawajibu watu, Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi, au kwa utawa wetu sisi? 13Mungu wa Ibrahimu na Isaak na Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambae ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe. 14Ninyi mlimkana yule Mtakatifu, yule Mwenye haki, mkataka mpewe muuaji: 15mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambae Mungu amemfufua: na sisi tu mashahidi wake. 16Na kwa imani ya jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnaemwona na kumjua: na imani ile iliyo kwa njia yake yeye imempatia huyu mbele yemi ninyi nyote uzima huu mkamilifu. 17Bassi sasa ndugu, najua ya kuwa mliyatenda haya kwa kutokujua kwenu, kama na wakuu wenu walivyotenda. 18Lakini mambo yale aliyokhubiri Mungu tangu zamani kwa vinywa vya manabii wake wote, ya kama Kristo atateswa, ameyatimiza hivyo. 19Tubuni bassi, mrejee, illi dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuhurudishwa kwa kuwako kwake Bwana: 20apate kumtuma Kristo aliyekhubiriwa kwenu tangu zamani; 21ambae ilimpasa kupokewa mbinguni hatta zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa vinywa vya manabii wake tokea mwanzo wa ulimwengu. 22Kwa maana Musa aliwaambia baba zetu ya kama, Bwana Mungu atawainulieni nabii, atakaetoka katika ndugu zenu, kama mimi, msikieni yeye katika mambo yote atakayonena. 23Na itakuwa ya kwamba kilia mtu asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake. 24Naam, na manabii wote tangu Samwil na wale waliokuja nyuma yake, wote walionena, walikhubiri khabari za siku hizi. 25Ninyi m watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na baba zenu, akimwambia Ibrahimu, Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa. 26Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, illi kuwabarikini kwa kumwepusha killa mmoja wenu na maovu wake.
Iliyochaguliwa sasa
Matendo 3: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.