Matendo 2
2
1HATTA ilipotimia siku ya Pentekote walikuwako wote pamoja mahali pamoja. 2Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kassi, ukaijaza nyumba yote walipokuwa wameketi. 3Kukawatokea ndimi zilizogawanyika, kama ndimi za moto uliowakalia killa mmoja wao. 4Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha mbalimbali, kama Roho alivyowajalia kutamka. 5Na walikuwako Yerusalemi Wayahudi wakikaa, watu watawa, watu wa killa taifa chini ya uwingu. 6Bassi sauti hii ilipokuja makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa killa mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake. 7Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Si hawa wote wasemao Wagalilaya? 8Imekuwaje bassi sisi kusikia killa mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? 9Waparthi na Wamedi na Waelamiti, nao wakaao Mesopotamia, Yahudi ua Kappadokia, Ponto na Asia, 10Frugia na Pamfulia, Misri na pande za Libua karibu na Kurene, na Warumi wageni, Wayahudi na Waongofu, 11Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa maneno yetu matendo makuu ya Mungu.
12Wakashangaa wote wakaingiwa na mashaka, wakaambiana, Maana yake nini mambo haya? 13Wengine walidhihaki, wakisema, Wamelewa kwa mvinyo mpya.
14Lakini Petro akasimama pamoja na wale edashara, akapaaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemi, jambo hili lijulike kwenu, mkasikilize maneno yangu. 15Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana; 16lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoel:
17Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu,
Nitawamwagia watu wote Roho yangu,
Na wana wenu na binti zenu watatabiri,
Na vijana wenu wataona maono:
Na wazee wenu wataota ndoto:
18Na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wauawake Roho yangu,
Nao watatabiri,
19Nitatoa ajabu katika mbingu juu,
Na ishara katika inchi chini,
Damu na moto, na mvuke wa moshi:
20Jua litageuka kuwa giza,
Na mwezi kuwa damu,
Kabla ya kuja ile siku ya Bwana
Iliyo kuu, dhahiri.
21Na itakuwa killa atakaeliitia jiua la Bwana ataokolewa.
22Enyi waume wa Israeli, sikieni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua; 23mtu huyu alitwaliwa nanyi kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake taugu zamani, nanyi mkamsulibisha kwa mikono mibaya, mkamwua: 24Mungu akamfufua, akilegeza utungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao. 25Maana Daud amtaja khabari zake,
Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote,
Kwa kuwa yuko mkono wangu wa kuume, nisitikisike.
26Kwa hiyo moyo wangu ukapendezwa, ulimi wangu ukafurahi;
Tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini.
27Kwa maana hutaniacha roho yangu katika kuzimu:
Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu.
28Umenifundisha njia ya uzima;
Utanijaza furaha kwa uso wako.
29Ndugu, mniwie radhi, niseme pasipo khofu mbele yenu khabari za baba yetu mkuu Daud, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hatta leo. 30Bassi kwa kuwa nabii, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa viuno vyake kwa jinsi ya kiwiliwili atamwinua Kristo, akae katika kiti chake cha enzi; yeye mwenyewe 31akitangulia kuyaona haya, alitaja khabari za kufufuka kwake Kristo, ya kama roho yake haikuachwa katika kuzimu, wala mwili wake hankuona uharibifu, 32Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake. 33Bassi akiisha kupandishwa hatta mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia. 34Maana Daud hakupanda mbinguni: bali yeye mwenyewe amesema,
Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti mkono wangu wa kuume.
35Hatta nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.
36Bassi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.
37Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe killa mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na watoto wenu, na watu wote walio mbali, na wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu. 40Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. 41Nao waliolipokea neno lake kwa furaha wakabatizwa: na siku ile wakazidishiwa watu wapata elfu tatu. 42Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.
43Killa mtu akaingiwa na khofu: ajabu nyingi na ishara zikafanyika kwa ujumbe wa mitume. 44Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, 45wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama killa mtu alivyokuwa na haja. 46Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kupokea chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, 47wakimsifu Mungu, na kuwapendeza wutu wote. Bwana akalizidisha kanisa killa siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
Iliyochaguliwa sasa
Matendo 2: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.