Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kassi, ukaijaza nyumba yote walipokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyika, kama ndimi za moto uliowakalia killa mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha mbalimbali, kama Roho alivyowajalia kutamka.