Marko MT. 11
11
1HATTA walipokaribia Yerusalemi karibu na Bethfage na Bethania, kukabili mlima wa Mizeituni, akawatuma wawili katilia wanafunzi wake, akawaambia, 2Enendeni zenu hatta kile kijiji kinachowakahili. Katika kuingia ndani yake marra mtaona mwana punda amefungwa, asiyepandwa na mtu hado; mfungueni, kamleteni. 3Na mtu akiwaambieni, Mbona mnafanya hivi? semeni, Bwana ana haja nae; na marra atampeleka hapa. 4Wakaenda zao, wakamwona mwana punda amefungwa penye mlango, nje katika njia kuu, wakamfungua. 5Baadhi ya watu waliosimama huko wakawaamhia, Mnafanyani mkimfungua mwana punda? 6Wakawaambia kama Yesu alivyowaagiza. 7Wakamletea Yesu yule mwana punda, wakatandika mavazi yao juu yake; akaketi juu yake. 8Watu wengi wakatandaza mavazi yao njiani, wengine wakakata matawi ya miti na kuyatandaza njiani. 9Watu waliotangulia na wale waliofuata wakapaaza sauti zao, wakinena, Utuokoe sasa; amebarikiwa ajae kwa jina la Bwana; 10umebarikiwa ufalme ujao kwa jina la Bwana, ufalme wa baba yetu Daud. Utuokoe sasa, wewe uliye juu.
11Yesu akaingia Yerusalemi hatta ndani ya hekalu: na alipokwisha kutazama yote pande zote, kwa kuwa ni wakati wa jioni, akatoka akaenda Bethania pamoja na wathenashara.
12Hatta assubuhi yake walipotoka Bethania akaona njaa. 13Akaona toka mbali mtini wenye majani, akaenda illi labuda aone kitu juu yake: na alipofika hakuona kitu illa majani: 14maana haukuwa wakati wa tini. Yesu akajibu, akauambia, Tangu leo hatta milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia. 15Wakafika Yerusalemi, Yesu akaingia ndani ya hekalu, akaanza kuwafukuza watu waliokuwa wakiuza na kununua ndani ya hekalu, akazipindua meza za wabadilio fedha, na viti vyao wauzao njiwa; 16wala hakuacha mtu achukue chombo kati ya hekalu. 17Akafundisha, akiwaambia, Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali nanyi mmeifanya kuwa pango ya wanyangʼanyi. 18Waandishi na makuhani wakini wakapata khabari wakatafuta jinsi ya kumwangamiza: maami walimwogopa, kwa sababu makutano yote walishangaa kwa elimu yake. 19Na ilipokuwa jioni alitoka mjini. 20Na assubuhi walipokuwa wakipita, wakauona ule mtini umekauka tangu shina lake. 21Petro akakumbuka khabari yake, akamwabia, Rabbi, tazama, mtini ulioulaani umekauka. 22Yesu akajibu, akamwambia, Mwe na imani kwa Mungu, 23Amin, nawaambieni, Ye yote atakaenambia mlima huu, Ngʼoka ukatupwe baharini, asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yamekuwa, yatamtukia hayohayo aliyosema.
24Kwa sababu biyo nawaambieni, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea nayo yatakuwa yenu. 25Nanyi, killa msimamapo na kusali, sameheni, kama mkiwa na neno juu ya mtu: illi Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. 26La, kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.
27Wakafika Yerusalemi tena: hatta alipokuwa akitembea hekaluni, makuhani wakuu na waandishi na wuizee wakamwambia, 28Kwa mamlaka gani utendayo haya? Na ni nani aliyekupa mamlaka hii uyatende haya? 29Yesu akajibu akawaambia, Mimi nami nitawauliza neno moja, nanyi nijibuni, kiisha nitawaambieni kwa mamlaka gani nitendayo haya. 30Ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni au kwa wana Adamu? Nijibuni. 31Wakasemezana wao kwa wao, wakinena, Kama tukisema, Toka mbinguni, atasema, Mbona, bassi, hamkuniwamini? 32Bali tukisema, Ulitoka kwa wana Adamu—waliogopa watu: maana watu wote walimwona Yohana kuwa nabii kweli kweli. 33Wakamjibu Yesu, wakanena, Hatujui. Yesu akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi kwa mamlaka gani nitendayo haya.
Iliyochaguliwa sasa
Marko MT. 11: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.