Marko MT. 12
12
1AKAANZA kusema nao kwa mifano. Mtu alipanda mizabibu, akazungusha nzio, akachimbia shimo lake shinikizo, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. 2Hatta kwa wakati wake akatuma mtumwa kwa wale wakulima, illi apokee kwa wakulima baadhi ya matunda ya mizabibu. 3Wakamtwaa, wakampiga, wakamtoa nje, hana kitu. Akatuma tena kwao mtumwa mwingine. 4Na huyo wakampiga mawe, wakamtia jeraha ya kichwa, wakamtoa ametiwa aibu. 5Akamtuma mwingine, huyo wakamwua; na wengine wengi, wakiwapiga hawa, na wakiwana hawa. 6Bassi alikuwa na mwana mmoja bado, mpendwa wake; huyu nae akamtuma kwao wa mwisho, akinena, Watamjali mwana wangu. 7Wale wakulima wakasemezana, Huyu ni mrithi; haya, na tumwue, na urithi utakuwa wetu. 8Wakamkamata, wakamwua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu. 9Bassi atafanyani yule Bwana wa mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa watu wengine. 10Hatta andiko hili hamjalisoma?
Jiwe walilokataa waashi
Hili limekuwa jiwe kuu la pembeni.
11Neno hili limetoka kwa Bwana
Nalo ni ajabu machoni petu.
12Wakatafuta kumkamata, wakaogopa makutano; maana walitambua ya kwamba ule mfano amewanena wao. Wakamwacha wakaenda zao.
13Wakatuma kwake baadhi ya Mafarisayo na Maherodiano, illi wamnase kwa maneno. 14Hatta walipofika wakamwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu: lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! ni halali kumpa Kaisari kodi au sivyo? Tumpe, tusimpe? 15Nae, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? nileteeni dinari niione. Wakaleta. 16Akawaambia, Ya nani sanamu hii na anwani hii? 17Wakamwambia, Ya Kaisari. Yesu akajibu, akawaambia, Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu. Wakamtaajahia sana.
18Na Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hapana kiyama, wakamwendea, 19wakamwuliza wakinena, Mwalimu, Musa alituandikia ya kwamba ndugu ya mtu akifa, akamwacha mke wake wala hana mtoto, ndugu yake amtwae yule mke wake akampatie ndugu yake mzao. 20Bassi palikuwa na ndugu saba; wa kwanza akatwaa mke, akafa, asiache mzao. 21Wa pili nae akamtwaa akafa, wala yeye hakuacha mzao. 22Hatta na wa tatu kadhalika; wukamtwaa wote saba wasiache mzao. Mwisho wa wote yule mwanamke akafa nae. 23Bassi, katika kiyama watakapofufuka atakuwa mke wa nani katika hawa? Maana wote saba walikuwa nae. 24Yesu akajibu, akawaambia, Je! Hamjidanganyi kwa sababu hii, kwa kuwa bamyajui maandiko wala uweza wa Mungu? 25Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaozwi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni. 26Na katika khabari ya wafu ya kwamba wafufuka, hamjasoma katika Kitabu cha Musa, mwenye Kijiti, jinsi Mungu alivyomwambia, akinena, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaak, na Mungu wa Yakobo? 27Yeye si Mungu wa wafu, bali wa wahayi. Kwa hiyo mwajidanganya sana.
28Mmojawapo wa waandishi akafika, amewasikia wakisemezana nae, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ipi iliyo ya kwanza? 29Yesu akamjibu, Katika amri zote ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; 30nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Amri ya kwanza ndiyo hii. 31Na ya pili yafanana na bayo, ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hapana nyingine iliyo kuu kuliko hizi. 32Yule mwandishi akamwambia, Hakika, mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hapana mwingine illa yeye: 33na kumpenda kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa roho yote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko kafara zote na dhabihu zote. 34Yesu, alipoona kwamba amejibu kwa busara, akamwambia, Wewe huwi mbali na ufalme wa Mungu. Wala hakuthubutu mtu kumsaili neno tena tokea hapo. 35Hatta Yesu alipokuwa akifundisha katika hekalu, akajibu, akanena, Kwa maana gani waandishi hunena ya kwamba Kristo yu Mwana wa Daud? 36Kwa sababu Daud mwenyewe alisema, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu,
Bwana alimwambia Bwana wangu,
Keti mkono wangu wa kuume
Hatta niwafanyapo adui zako kuwa chini ya miguu yako.
37Daud mwenyewe amwita Bwana: bassi amekuwaje mwana wake? Na ule mkutano mkubwa walikuwa wakimsikiliza kwa furaha. 38Akawaambia katika mafundisho yake, Jibadharini na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni, 39na kukaa mbele katika sunagogi, na mahali pa mbele katika karamu: 40wanakula nyumba za wajane, na kwa unafiki husali sala ndefu: hawa watapokea hukumu iliyo kubwa.
41Yesu akaketi kuielekea sanduku ya hazina, akatazama jinsi makutano watiavyo fedha katika sanduku. Matajiri wengi wakatia vingi. 42Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia sarafu mbili za shaba, kiasi cha nussu pesa. 43Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambieni, Huyu mjane maskini ametia vingi kuliko wote wanaotia katika sanduku ya hazina: 44maana hawa wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi: bali huyu katika mahitaji yake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndio maisha yake yote pia.
Iliyochaguliwa sasa
Marko MT. 12: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.