Marko MT. 4
4
1AKAANZA kufundisha tena kando ya bahari. Wakamkusanyikia mkutano mkuliwa, hatta yeye akapanda chomboni, akakaa baharini; mkutano wote ulikuwako katika inchi kavu kando ya bahari. 2Akawafundisha mengi kwa mifano, akawaambia katika mafundisho yake, 3Sikilizeni: Mpanzi alitoka kwenda kupanda; 4ikawa alipokuwa akipanda, baadhi ya mbegu zikaangukia njiani, wakaja ndege wakazila. 5Nyingine zikaanguka penye mwamba, pasipokuwa na udongo mwingi; marra zikamea kwa kuwa na udongo haba; 6hatta jua lilipoznka zikaungua, na kwa kuwa hazina mizizi zikakauka. 7Nyingine zikaanguka penye miiba: ile miiba ikakua, ikazisonga, zisizae matunda. 8Nyingine zikaanguka panapo udongo ulio mzuri, zikazaa matunda, zikimea na kukua, na kuzaa, moja thelathini, moja sittini, na moja mia. 9Akanena, Aliye na masikio ya kusikilia, na asikie.
10Alipokuwa peke yake, watu waliomzunguka, na wale thenashara wakamwuliza khabari za ule mfano. 11Akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuijua siri ya ufalme wa Mungu; hali wale walio nje yote huwawia kwa mifano, 12illi wakitazama watazame, wasione; na wakisikia wasikie, wasifahamu; wasije wakageuka, wakasamehewa dbambi zao.
13Askawaambia, Hamjui mfano huu? Bassi mifano yote mtaitambuaje? 14Mpanzi yule hulipanda neno. 15Hawa ndio walio njiani, lipandwapo neno; nao, wakiisha kusikia, marra huja Shetani, akaliondoa lile neno lililopandwa mioyoni mwao. 16Kadhalika na hawa ndio wapandwao penye mwamba, ambao kwamba wakiisha kulisikia lile neno, marra hulipokea kwa furaha; 17waki hawana mizizi ndani yao, hali hudumu muda mehache; kiisha ikitokea shidda au udhia kwa sababu ya lile neno, marra huchukizwa. 18Na hawa ndio wale wapandwao penye miiba, ni watu walisikiao lile neno, 19na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga lile neno, likawa halizai. 20Na hawa ndio waliopandwa panapo udongo mzuri; ni watu walisikiao lile neno na kulipokea, na kuzaa matunda, moja thelathini, moja sittini, na moja mia. 21Akawaambia, Mwaonaje? Taa huletwa illi kutiwa ehini ya kikapu, au ehini ya kitanda? si kutiwa juu ya kibao cha kuwekea taa? 22Kwa maana hakuna neno lililostirika, illa kusudi lije likadhihirika; wala halikuwa siri, illa kusudi lije likatokea dhahiri. 23Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie. 24Akawaambia, Tafakarini msikialo, kipimo mpimacho mtapimiwa kile kile, na bado mtazidishiwa. 25Kwa maana mtu aliye na kitu atapewa, nae asiye na kitu, hatta kile alicho nacho ataondolewa.
26Akanena, Ufalme wa Mungu, mithili yake ni mtu aliyemwaga mbegu juu ya inchi: 27akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikimea na kukua, asivyojua yeye. 28Maana inchi huzaa yenyewe, kwanza jani, tena suke, kiisha nganu mpevu katika suke. 29Hatta matunda yakiiva, marra aupeleka mundu kwa kuwa mavuno yamewadia.
30Akanena, Tuulinganishe na nini ufalme wa Mungu? au tuutie katika mfano gani? 31Ni kama punje ya kharadali ambayo, ipandwapo katika inchi, ni ndogo kuliko mbegu zote zilizo katika inchi, 32na ikiisha kupandwa, hukua, ikawa kubwa kuliko miti yote ya mboga, ikifanya matawi makuhwa; hatta ndege za anga waweza kukaa chini ya uvuli wake.
33Kwa mifano mingi ya namna hii alikuwa akisema nao neno lake, kwa kadiri walivyoweza kusikia; 34wala pasipo mfano hakusema nao: akawaeleza wanafunzi wake mambo yote kwa faragha. 35Siku ile ilipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke hatta ngʼambu. 36Wakawaacha makutano, wakamchukua vile vile katika chomho kile kile. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja nae. 37Ikatokea dharuba kuu ya npepo, mawimbi yakapiga chombo hatta kikaanza kujaa maji. 38Yeye mwenyewe alikuwa katika shetri, amelala juu ya mto: wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunapotea? 39Akaamka: akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, tulia. Upepo nkakoma, kukuwa shwari kuu. 40Akawaambia, Mbona mu waoga? Hamna imani bado? 41Wakaingizwa na khofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, bassi, hatta upepo na bahari zamtii?
Iliyochaguliwa sasa
Marko MT. 4: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.