2 Mose 1
1
Kusumbuliwa kwao Waisiraeli.
1Haya ndiyo majina yao wana wa Isiraeli walioingia Misri; nao walikuja pamoja na Yakobo, kila mtu na mlango wake.#1 Mose 46:8. 2Rubeni, Simeoni, Lawi na Yuda, 3Isakari, Zebuluni na Benyamini, 4Dani na Nafutali, Gadi na Aseri. 5Wao wote waliotoka viunoni mwa Yakobo walikuwa watu 70. Naye Yosefu alikuwa yuko kule Misri.#1 Mose 46:27. 6Yosefu alipokwisha kufa na ndugu zake wote nacho hicho kizazi chote,#1 Mose 50:26. 7wana wa Isiraeli wakazaa wana, wakazidi kuwa wengi na wenye nguvu sanasana, wakajieneza katika nchi hiyo.#Tume. 7:17.
8Kisha akaondokea mfalme mpya asiyemjua Yosefu. 9Naye akawaambia watu wake: Tazameni! Ukoo wa wana wa isiraeli unatushinda kwa wingi na kwa nguvu. 10Na tuwaendee kwa werevu, wasizidi kuwa wengi. Kwani itakuwa, vita vitakapotupata, watarudi upande wa adui zetu, wapigane nasi, wapate kuiteka nchi hii. 11Kwa hiyo wakawawekea wasimamizi wakali, wawatese na kuwafanyisha kazi ngumu, wakamjengea Farao miji ya kulimbikia vyo vyote, ndio Pitomu na Ramusesi.#1 Mose 15:13; 47:11. 12Lakini hivyo, walivyowatesa, ndivyo, walivyoendelea kuwa wengi na kuenea po pote, kwa hiyo wana wa Isiraeli wakawa kama tapisho kwao Wamisri, 13nao wakawafanyisha wana wa Isiraeli kazi za utumwa na kuwakorofisha. 14Wakawakalisha kuwa wenye uchungu siku zote kwa kuwafanyisha kazi ngumu za utumwa za kuumba na za kuchoma matofali na za kulima mashamba; hivyo wakawafanyisha kazi zo zote za utumwa za kuwatumikia, wakiwakorofisha.
15Kisha mfalme wa Misri akawaagiza wazalishaji wa Kiebureo, mmoja jina lake Sifura, wa pili jina lake Pua, 16kwamba: Mkiwazalisha wanawake wa Kiebureo waangalieni, wakizaa! Kama mtoto ni wa kiume, sharti mmwue, lakini kama mtoto ni wa kike, na apone! 17Lakini hao wazalishaji wakamwogopa Mungu, hawakufanya, kama mfalme wa Misri alivyowaagiza, wakawaacha watoto, wapone. 18Ndipo, mfalme wa Misri alipowaita wale wazalishaji, akawauliza: Mbona mnafanya hivyo mkiwaacha watoto, wapone? 19Nao wazalishaji wakamwambia Farao: Ni kwa kuwa wanawake wa Kiebureo hawafanani na wanawake wa Kimisri, kwani wao wako na nguvu zaidi, mzalishaji akiwa hajafika bado kwao, wamekwisha kuzaa. 20Kwa hiyo Mungu akawafanyizia mema hao wazalishaji, nao watu wakaendelea kuwa wengi zaidi wenye nguvu. 21Kwa kuwa hao wazalishaji walimwogopa Mungu, akawajengea nyumba. 22Kisha Farao akawaagiza watu wake wote kwamba: Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa sharti mumtupe mtoni, lakini watoto wote wa kike na mwaache, wapone!
Iliyochaguliwa sasa
2 Mose 1: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.