1 Mose 50
50
Yakobo anazikwa Heburoni.
1Yosefu akamwangukia baba yake usoni, akamlilia na kumnonea.#1 Mose 46:4. 2Kisha Yosefu akawaagiza watumishi wake waganga, wampake baba yake manukato; ndipo, hao waganga walipompaka Isiraeli manukato, 3mpaka siku 40 zikitimia, kwani kuzitimiza hizo siku ndio desturi ya kupaka manukato. Nao Wamisri akamwombolezea siku 70.
4Siku za maombolezo zilipokwisha pita, Yosefu akawaambia wao wa nyumbani mwake Farao kwamba: Kama nimeona upendeleo machoni penu, semeni masikioni pake Farao ya kwamba: 5Baba yangu ameniapisha kwamba: Tazama! Mimi ninakufa; sharti unizike katika kaburi langu, nililojichimbia katika nchi ya kanaani. Sasa ninataka kupanda kwenda huko, nimzike baba yangu, kisha nirudi.#1 Mose 47:29-30. 6Naye Farao akasema: Panda kwenda huko, umzike baba yako, kama alivyokuapisha.
7Yosefu alipopanda kwenda huko kumzika baba yake, wakaenda naye watumwa wazee wote wa nyumbani mwake Farao nao wazee wote wa nchi ya Misri, 8nao wote wa mlango wa Yosefu nao ndugu zake nao wote wa mlango wa baba yake; watoto wao tu na mbuzi na kondoo na ng'ombe wao waliwaacha katika nchi ya Goseni. 9Nayo magari na wapanda farasi wakapanda naye, wakawa kikosi kikubwa sana. 10Walipofika pake Atadi pa kupuria ngano palipo ng'ambo ya huko ya Yordani wakafanya maombolezo makuu yenye vilio kabisa. Ndivyo, Yosefu alivyolala matanga siku saba kwa ajili ya baba yake. 11Wenyeji wa nchi ya Kanaani walipoyaona hayo matanga pake Atadi pa kupuria ngano wakasema: Matanga haya ya Wamisri ni makuu kweli, kwa sababu hii wakapaita jina lake mahali pale palipo ng'ambo ya huko ya Yordani: Tanga la Misri. 12Kisha wanawe wakayafanya yayo hayo, aliyowaagiza:#1 Mose 49:29. 13wao wanawe wakamchkua na kumpeleka katika nchi ya Kanaani, kisha wakamzika katika lile pango katika shamba la Makipela, ndilo shamba lile, Aburahamu alilolinunua kwa Mhiti Efuroni kuwa mahali pake pa kuzikia, napo palikuwa panaelekea Mamure.#1 Mose 23:16. 14Yosefu alipokwisha kumzika baba yake akarudi Misri, yeye na ndugu zake nao wote waliopanda naye kwenda kumzika baba yake.
Utu mwema wa Yosefu.
15Lakini kaka zake Yosefu wakaogopa, kwa kuwa baba yao amekufa, wakasema mioyoni: Labda Yosefu atatuchukia, atulipize mabaya, tuliyomfanyizia. 16Kwa hiyo wakatuma kwake Yosefu kumwambia kwamba: Baba yako alipokuwa hajafa bado alituagiza kwamba: 17Hivi ndivyo, mtakavyomwambia Yosefu: E ndugu, yaondoe mapotovu na makosa yao ndugu zako! Kwani walikufanyizia mabaya. Sasa waondolee watumishi wa Mungu wa baba yako hayo mapotovu! Yosefu akalia machozi, walipomwambia maneno haya. 18Kisha kaka zake wenyewe wakaenda, wakamwangukia na kumwambia: Sisi hapa tu watumwa wako. 19Lakini Yosefu akawaambia: Msiogope! Je? Mimi ninapashika mahali pake Mungu? 20Kweli ninyi mwaliwaza kunifanyizia mabaya, lakini Mungu aliyageuza kuwa mema, ayafanye yaliyo waziwazi leo, aponye watu wengi.#1 Mose 45:5; Yes. 28:29. 21Kwa hiyo msiogope sasa! Mimi nitawatunza ninyi na watoto wenu. Hivyo akawatuliza mioyo akisema nao kwa upole.
22Yosefu akakaa Misri, yeye pamoja nao walio wa mlango wa baba yake; nayo miaka yake Yosefu ya kuwapo ilikuwa 110. 23Yosefu akaona wana wa Efuraimu hata kizazi cha tatu, nao wana wa Makiri, mwana wa Manase, wakazaliwa magotini pake Yosefu.#1 Mose 30:3.
Kufa kwake Yosefu.
24Kisha Yosefu akawaambia ndugu zake: Mimi ninakufa, lakini ninyi Mungu atawapatia njia ya kuwatoa katika nchi hii na kuwapandisha kwenda katika hiyo nchi, aliyowaapia akina Aburahamu na Isaka na Yakobo kuwapa.#Ebr. 11:22. 25Kisha Yosefu akawaapisha wana wa Isiraeli kwamba: Hapo, Mungu atakapowakagua ninyi, sharti mwichukue mifupa yangu kwenda nayo!#2 Mose 13:19; Yos. 24:32. 26Kisha Yosefu akafa mwenye miaka 110, wakampaka manukato, wakamweka ndani ya sanduku huko Misri.
Iliyochaguliwa sasa
1 Mose 50: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.