2 Mose 22
22
Mapatilizo ya wezi.
1Mtu akiiba ng'ombe au kondoo, akimchinja au akimwuza, kwa ng'ombe mmoja sharti alipe ng'ombe watano, na kwa kondoo mmoja sharti alipe kondoo wanne.#Luk. 19:8. 2Mwizi akikamatwa papo hapo, anapovunjia nyumba, akipigwa, afe, basi, siko kukora manza za damu. 3Lakini kama jua lilikuwa limekwisha kucha tangu hapo, mwenye kumwua atakuwa amekora manza za damu. Mwizi hana budi kuyalipa aliyokwiba; akiwa hanayo malipo, na auzwe kwa ajili ya wizi wake. 4Kama nyama, aliyemwiba, anapatikana mkononi mwake angali mzima, kama ni ng'ombe au punda au kondoo, sharti alipe wawili.
Mapatilizo yao wanaoharibu mali za watu na mengine.
5Mtu akilisha shamba au mizabibu, akiliacha kundi lake, lijiendee kulisha shambani kwa mwingine, sharti amlipe na kuyatoa mazao ya shamba lake yeye na ya mizabibu yake yeye yaliyo mema. 6Moto ukitoka kwenye kuchoma miiba, ukala miganda iliyokwisha kufungwa au mabua yenye ngano au shamba lo lote, basi, mwenye kuuwasha huo moto sharti ayalipe yaliyoharibika.
7Mtu akimpa mwenzake fedha au vyombo, amwekee, navyo vikiibiwa nyumbani mwa mwenzake, mwizi akionekana, sharti avilipe mara mbili. 8Lakini mwizi asipoonekana, mwenye nyumba na apelekwe kwa Mungu, waone, kama siye mwenyewe aliyevichukua vyombo vya mwenzake kwa mkono wake.#2 Mose 21:6. 9Shauri lo lote, mtu atakalomshtakia mwenzake, kama ni la ng'ombe au la punda au la kondoo au la nguo au la cho chote kilichopotea, mmoja akisema, ni mali yake yeye, basi, shauri lao hao wawili lipelekwe kwa Mungu; naye, Mungu atakayemtokeza kuwa mwenye kukosa, sharti amlipe mwenzake mara mbili kilichompotea.
10Mtu akimpa mwenzake ng'ombe au punda au kondoo au nyama wo wote wa kufuga, amtunzie, naye akafa au akaumia au akachukuliwa, mtu asione, 11mwenyewe na amwapishe mwenzake, amtaje Bwana kwamba hakuchukua mali ya mwenzake kwa mkono wake, kisha yule, mwenzake hana budi kumwitikia, asilipe. 12Lakini mwizi akimwiba kwake, sharti amlipe yule mwenyewe. 13Akiraruliwa na nyama, sharti amlete huyo nyama aliyeraruliwa kuwa ushahidi; basi, hivyo hatamlipa aliyeraruliwa.#1 Mose 31:39.
14Mtu akikopa nyama kwa mwenzake, naye huyo nyama akiumia au akifa, bwana wake akiwa hayuko, yule hana budi kumlipa. 15Kama bwana wake yuko hapo, halipi; kama alimkodisha huyo nyama, malipo yamo katika hizo fedha za kukodisha.
16Mtu akimdanganya mwanamwali asiyeposwa, alale naye, sharti amlipie mali za ukwe, awe mkewe.#5 Mose 22:28-29. 17Baba yake akikataa kabisa kumpa kuwa mkewe, bsi, atatoa fedha zimpasazo mwanamwali za posa.
18Mwanamke mlozi usimwache, awepo!#3 Mose 20:6,27; 5 Mose 18:10; 1 Sam. 28:9.
19Kila atakayelala na nyama sharti auawe kabisa.#3 Mose 18:23; 5 Mose 27:21.
20Mtu atakayetambikia miungu mingine, isipokuwa Bwana peke yake, sharti atiwe mwiko wa kuwapo.#5 Mose 13:6-18; 17:2-7.
21Mgeni usimwonee wala usimkorofishe! Kwani nanyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.#2 Mose 23:9. 22Mjane au mtoto aliyefiwa na wazazi usimtese!#3 Mose 19:33-34. 23Utakapomtesa atanililia mimi, mimi nami nitakisikia vema kilio chake.#5 Mose 10:18-19; 24:17-18; 27:19. 24Ndipo, makali yangu yatakapowaka moto, niwaue ninyi kwa upanga, wake zenu wawe wajane, nao watoto wenu wasiwe na baba tena.#Yes. 1:17.
25Ukiwakopesha fedha watu wa ukoo wangu, wakikaa kwako wenye ukosefu, usiwawie kama wakopeshaji wengine, ni kwamba: Msiwatoze faida kubwa za kukopesha!#3 Mose 25:36; 5 Mose 23:19; 24:10. 26Ukimtoza mwenzako blanketi lake kuwa rehani, sharti umrudishie, mpaka jua likichwa.#5 Mose 24:12-13. 27Kwani hulitumia la kujifunika, hili peke yake ni nguo yake ya kuufunika mwili wake; asipokuwa nalo atalalia nini? Naye atakaponililia, mimi nitamsikia, kwani mimi ni mwenye huruma.
28Mungu usimtukane! Wala mtawala ukoo wako usimwambie maovu!#2 Mose 21:6; Mbiu. 10:20; Tume. 23:5. 29Usikawilie kutoa malimbuko ya vilaji vyako vingi na ya vinywaji vyako! Naye mwanao wa kwanza unipe, awe wangu!#5 Mose 18:4; 2 Mose 13:2,13. 30vivyo hivyo sharti uvifanye hata kwa ng'ombe wako na kwa mbuzi na kondoo wako: wana wao wa kwanza na wakae na mama zao siku saba, siku ya nane uwatoe kunipa mimi!#3 Mose 22:27. 31Nanyi sharti mwe watu wangu watakatifu, msile nyama aliyeraruliwa porini, nyama zake sharti mwatupie mbwa.#3 Mose 7:24; 11:40; 17:15; 22:8; 5 Mose 14:21; Ez. 44:31.
Iliyochaguliwa sasa
2 Mose 22: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.