1 Mose 45
45
Yosefu anajitambulisha kwa ndugu zake.
1Yosefu asipoweza kuvumilia tena kwa ajili yao wote waliosimama kwake, ndipo alipoita kwamba: Watoeni wote humu mwangu! Kwa hiyo hakusimama mtu mwake, Yosefu alipojitambulisha kwa ndugu zake. 2Lakini alipopaza sauti kwa kulia, Wamisri wakavisikia, nao wa nyumbani mwa Farao wakavisikia. 3Kisha Yosefu akawaambia ndugu zake: Ni mimi Yosefu! Baba yangu yuko mzima bado? Lakini ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwani walimstukia. 4Ndipo, Yosefu alipowaambia ndugu zake: Nifikieni karibu! Nao walipokwisha kumkaribia, akawaambia: Ni mimi ndugu yenu Yosefu, mliyemwuza kupelekwa Misri.#1 Mose 37:28. 5Lakini sasa msisikitike, wala msijikasirikie, ya kuwa mliniuza kupelekwa huku! Kwani Mungu ndiye aliyenituma kwenda mbele yenu, nipate kuwaponya.#1 Mose 50:20. 6Kwani huu ni mwaka wa pili wa kuingia njaa katika nchi hii, ingaliko miaka mitano isiyo na kulima wala kuvuna. 7Kwa hiyo Mungu alinituma kwenda mbele yenu, niwapatie ninyi masao katika nchi hii na wokovu mkubwa wa kuwaponya ninyi. 8Sasa sio ninyi mlionituma kuja huku, ila ni Mungu mwenyewe. Naye akaniweka kuwa baba yake Farao na bwana wa nyumba yake yote na mtawala nchi zote za Misri.#1 Mose 41:40-43. 9Pigeni mbio, mpande kwenda kwa baba yangu, mmwambie: Hivi ndivyo, anavyosema mwanao Yosefu: Mungu ameniweka kuwa bwana wa nchi yote nzima ya Misri; telemka kuja kwangu, usikawilie! 10Na ukae katika nchi ya Goseni, upate kuwa karibu yangu, wewe na wanao na wana wa wanao na mbuzi na kondoo wako na ng'ombe wako navyo vyote, ulivyo navyo. 11Nitakutunza huku, kwani ingaliko bado miaka mitano ya njaa; zisiangamizwe mali zako wewe nazo zao walio wa mlango wako, nazo zao wote, ulio nao. 12Macho yenu ninyi yanaona, nayo macho ya ndugu yangu Benyamini yanaona, ya kuwa ni kinywa changu mimi kinachosema nanyi. 13Msimulieni baba yangu, utukufu wangu wote ulivyo huku Misri, nayo yote, mliyoyaona! Pigeni mbio, mmtelemshe baba yangu kuja huku! 14Kisha akamkumbatia nduguye Benyamini, akali machozi; Benyamini naye akalia machozi shingoni pake. 15Nao kaka zake wote akanoneana nao pamoja na kulia machozi; kisha kaka zake wakaongea naye.
Yosefu anawatuma kaka zake kumchukua Yakobo.
16Uvumi uliposikilika nyumbani mwa Farao kwamba: Ndugu zake Yosefu wamefika! akapendezwa Farao nao watumishi wake. 17Naye Farao akamwambia Yosefu: Waaambie ndugu zako: Fanyeni hivi: wachukuzeni nyama wenu mizigo, mpate kwenda zenu! Mtakapofika katika nchi ya Kanaani, 18mchukueni baba yenu nao wa milango yenu, mje kwangu! Nitwapa kipande cha nchi ya Misri kilicho kizuri, mle manono ya nchi hii! 19Wewe umekwisha kuagizwa, uwaambie: Fanyeni hivi: jichukulieni huku katika nchi ya Misri magari ya kuwachukulia watoto wenu na wake zenu! Naye baba yenu mchukueni, mje naye! 20Msijiumize kwa ajili ya vyombo vyenu! Kwani mema yote ya nchi nzima ya Misri ni yenu! 21Nao wana wa Isiraeli wakafanya hivyo, maana Yosefu akawapa magari kwa ile amri ya Farao, akawapa nazo pamba za njiani. 22Nao wote akawapa nguo za zikukuu, kila mmoja yake; lakini Benyamini akampa fedha 300 na nguo tano za sikukuu. 23Naye baba yake akampelekea vitu hivi: punda kumi waliochukua vitu vizuri vya Misri na majike ya punda kumi waliochukua ngano na chakula kingine na pamba za njiani za baba yake. 24Alipoagana na ndugu zake, waende zao, akawaambia: Msigombane njiani!#1 Mose 42:22.
25Ndivyo, walivyotoka Misri, wapande kwenda katika nchi ya Kanaani kwa baba yao Yakobo. 26Wakamsimulia kwamba: Yosefu yuko mzima bado, naye ndiye anayeitawala nchi yote nzima ya Misri; lakini moyo wake ukapigwa bumbuazi, hakuyategemea maneno yao. 27Wakamwambia maneno yote, Yosefu aliyowaambia; naye alipoyaona hayo magari, Yosefu aliyoyatuma kumchukua, ndipo, roho yake ilipomrudia baba yao Yakobo. 28Kisha Isiraeli akasema: Lililo kuu ni hili: mwanangu Yosefu angaliko mzima. Nitakwenda, nimwone, kabla sijafa.#1 Mose 46:30.
Iliyochaguliwa sasa
1 Mose 45: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.