1 Mose 46
46
Yakobo anakwenda kukaa Misri.
1Isiraeli akaondoka pamoja nayo yote, aliyokuwa nayo, akaja Beri-Seba; ndiko, alikomchinjia Mungu wa baba yake Isaka ng'ombe za tambiko.#1 Mose 26:23-25. 2Naye Mungu akamtokea Isiraeli usiku, akamwita kwamba: Yakobo! Yakobo! Akaitikia: Mimi hapa! 3Naye akamwambia: Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako; usiogope kutelemka Misri! Kwani ndiko, nitakakokupa kuwa taifa kubwa. 4Mimi nitatelemka pamoja na wewe kwenda Misri, nami nitakupandisha tena kuja huku, naye Yosefu atayafumba macho yako kwa mkono wake. 5Yakobo alipoondoka Beri-Seba, wana wa Isiraeli wakampandisha baba yao Yakobo garini nao watoto wao na wake zao, ndiyo yale magari, Farao aliyoyatuma kumchukua. 6Wakayachukua nayo makundi yao na mapato yao, waliyoyapata katika nchi ya Kanaani, wakafika Misri, yeye Yakobo nao wa uzao wake wote pamoja naye. 7Wanawe na wajukuu wake nao wanawe wa kike na wajukuu wake wa kike nao wa uzao wake wote aliwapeleka Misri kwenda naye.
Vizazi vyake Isiraeli.
8Haya ndiyo majina ya wana wa Isiraeli waliokwenda Misri. Yakobo na wanawe: Mwana wa kwanza wa Yakobo ni Rubeni.#2 Mose 6:14-16. 9Nao wana wa Rubeni ni Henoki na Palu na Hesironi na Karmi. 10Nao wana wa Simeoni ni Yemueli na Yamini na Ohadi na Yakini na sohari na Sauli, mwana wa mwanamke wa Kanaani. 11Nao wana wa Lawi ni Gersoni na Kehati na Merari.#2 Mose 6:16. 12Nao wana wa Yuda ni Eri na Onani na Sela na Peresi na Zera; lakini Eri na Onani walikuwa wamekufa katika nchi ya Kanaani. Nao wana wa peresi walikuwa Hesironi na Hamuli.#1 Mose 38:3-4; 29:30. 13Nao wana wa Isakari ni Tola na Puwa na Yobu na Simuroni. 14Nao wana wa Zebuluni ni Seredi na Eloni na Yaleli. 15Hawa ndio wana wa Lea, aliomzalia Yakobo huko Mesopotamia, naye mwanawe wa kike ni Dina. Wanawe wote pamoja, wa kiume na wa kike, ni watu 33.
16Nao wana wa Gadi ni Sifioni na Hagi na suni na Esiboni, tena Eri na Arodi na Areli. 17Nao wana wa Aseri ni Imuna na Isiwa na Iswi na Beria na umbu lao Sera; nao wana wa Beria ni Heberi na Malkieli. 18Hawa ndio wana wa Zilpa, Labani aliyempa mwanawe Lea; naye alimzalia Yakobo hawa watu 16.
19Wana wa Raheli, mkewe Yakobo, ni Yosefu na Benyamini#1 Mose 41:50-52. 20Naye Yosefu katika nchi ya Misri alizaliwa Manase na Efuraimu; ndio, aliomzalia Asenati, binti Potifera, mtambikaji wa Oni. 21Nao wana wa Benyamini ni Bela na Bekeri na Asibeli, Gera na Namani, Ehi na Rosi, Mupimu na Hupimu na Ardi. 22Hawa ndio wana wa Raheli, Yakobo aliozaliwa; wote pamoja ni watu 14.
23Nao wana wa Dani ni Husimu. 24Nao wana wa Nafutali ni Yaseli na Guni na Yeseri na Silemu. 25Hawa ndio wana wa Biliha, Labani aliyempa mwanawe Raheli; naye alimzalia Yakobo hawa watu 7.
26Watu wote waliokwenda Misri na Yakobo ni 66; ndio waliotoka kiunoni mwake, tena wake zao wana wa Yakobo. 27Nao wana wa Yosefu aliozaliwa huko Misri, ni watu wawili; hivyo watu wote pia wa mlango wa Yakobo waliokuja Misri walikuwa 70.#2 Mose 1:5.
Yosefu anampokea baba yake Yakobo.
28Yakobo akamtuma Yuda kwenda mbele yake kwa Yosefu, amwonyeshe nchi ya Goseni, kisha wakaiingia hiyo nchi ya Goseni.#1 Mose 45:10. 29Ndipo, Yosefu alipolitandika gari lake, akamwendea baba yake Isiraeli huko Goseni. Alipomwonekea, akamkumbatia shingoni akalia machozi hapo shingoni pake kitambo kizima. 30Kisha Isiraeli akamwambia Yosefu: Sasa na nife, kwani nimekwisha kuuona uso wako, ya kuwa u mzima bado.#1 Mose 45:28.
31Kisha Yosefu akawaambia ndugu zake nao wa mlango wa baba yake: Nitapanda kumpasha Farao habari ya kwamba: Ndugu zangu nao wa mlango wa baba yangu waliokaa katika nchi ya Kanaani wamefika kwangu. 32Nao watu hawa ni wachungaji, kwani ni wenye makundi, nao mbuzi na kondoo wao na ng'ombe wao nayo yote, waliyokuwa nayo, wameyaleta huku. 33Naye Farao atakapowaita na kuwauliza: Kazi yenu nini? 34na mmwambie: Watumwa wako ni wachungaji tangu ujana wetu mpaka sasa; nasi tulivyo, ndivyo, nao baba zetu walivyokuwa, kusudi mpate kukaa katika nchi ya Goseni; kwani Wamisri huwachukiza wachungaji wote.#1 Mose 43:32.
Iliyochaguliwa sasa
1 Mose 46: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.