Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mose 48

48
Yakobo anambariki Efuraimu na Manase.
1Ikawa, mambo hayo yalipokwisha, wakamwambia Yosefu: Tazama! Baba yako ni mgonjwa. Ndipo, alipowachukua wanawe wawili Manase na Efuraimu kwenda naye. 2Walipompasha Yakobo habari kwamba: Tazama! Mwanao Yosefu anakuja kwako, Isiraeli akajitia nguvu, apate kukaa kitandani. 3Yakobo akamwambia Yosefu: Mwenyezi Mungu alinitokea Luzi katika nchi ya Kanaani, akanibariki,#1 Mose 28:19. 4akaniambia: Utaniona, nikikupa kuzaa wana, nikupe kuwa wengi, uwe mkutano wa makabila ya watu; kisha nchi hii nitawapa wao wa uzao wako wajao nyuma yako, mwichukue kuwa yenu kale na kale.#1 Mose 35:11-12. 5Sasa wanao wawili uliowazaa katika nchi hii ya Misri, nilipokuwa sijafika huku Misri, ni wangu; Efuraimu na Manase watakuwa wangu, kama Rubeni na Simeoni walivyo wangu,#1 Mose 41:50-52. 6nao wanao wengine, utakaowazaa nyuma yao, watakuwa wako; lakini wale wataitwa pamoja na majina ya ndugu zao, wagawiwe nao mafungu yao ya nchi yatakayokuwa yao. 7Nami nilipotoka Mesopotamia nilifiwa na Raheli njiani katika nchi ya Kanaani, uliposalia mwendo wa kipande kifupi tu kufika Efurata, nami nikamzika huko kwenye njia ya kwenda Efurata, ndio Beti-Lehemu.#1 Mose 35:19.
8Isiraeli alipowaona wana wa Yosefu akauliza: Hawa ni nani? 9Yosefu akamwambia baba yake: Ndio wanangu, Mungu alionipa huku; ndipo, alipomwambia: Walete kwangu niwabariki!#1 Mose 33:5. 10Maana macho yake Isiraeli yalikuwa yameguiwa na kiza, hayakuweza kuona kwa ajili ya uzee. Yosefu alipowafikisha karibu yake, akawanonea na kuwakumbatia. 11Kisha Isiraeli akamwambia Yosefu: Mimi sikuyawaza, ya kwamba nitauona uso wako, tena tazama! Mungu amenipa kuwaona nao wa uzao wako!#1 Mose 37:33,35; 45:26; Sh. 128:6. 12Ndipo, Yosefu alipowaondoa magotini pake, akamwinamia na kuufikisha uso wake chini. 13Kisha Yosefu akawachukua wote wawili, Efuraimu kwa mkono wake wa kuume na kumweka kushotoni kwake Isiraeli, naye Manase kwa mkono wake wa kushoto na kumweka kuumeni kwake Isiraeli; ndivyo, alivyowapeleka kwake. 14Lakini Isiraeli akaupeleka mkono wake wa kuuume, akaubandika kichwani pake Efuraimu aliyekuwa mdogo, nao mkono wake wa kushoto akaubandika kichwani pake Manase, naye akavifanya kusudi akiwabandikia mikono hivyo, kwani Manase ndiye aliyezaliwa wa kwanza. 15Kisha akambariki Yosefu na kusema: Mungu, ambaye baba yangu Aburahamu na Isaka walifanya mwenendo machoni pake, yeye Mungu alikuwa mchungaji wangu tangu hapo, nilipozaliwa, mpaka siku hii ya leo;#1 Mose 32:9; Sh. 23:1. 16naye malaika aliyenikomboa katika mabaya yote na awabariki hawa vijana, jina langu nayo majina ya baba zangu Aburahamu na Isaka yatajwe kwao, wawe wengi sana katika nchi hii!#1 Mose 31:11-13. 17Yosefu alipoona, ya kuwa baba yake ameubandika mkono wake wa kuume kichwani pake Efuraimu hakupendezwa; kwa hiyo akaushika huo mkono wa baba yake, auondoe kichwani pake Efuraimu, apate kuubandika kichwani pake Manase. 18Naye Yosefu akamwambia baba yake: Hivi sivyo, baba, kwani huyu ni wa kwanza; ubandike mkono wako wa kuume kichwani pake! 19Lakini baba yake akakataa akisema: Navijua, mwanangu, navijua kweli; huyu naye atakuwa kabila la watu, huyu naye atakuwa mkubwa, lakini ndugu yake mdogo atakuwa mkubwa kuliko yeye, nao wa uzao wake watakuwa mataifa mengi.#4 Mose 1:33,35; 5 Mose 33:17. 20Kisha akawabariki siku hiyo kwamba: Mwisiraeli atakapobariki atalitaja jina lako kwamba: Mungu na akupe kuwa kama Efuraimu na kama Manase! Hapa napo akamtaja Efuraimu mbele ya Manase.#Ebr. 11:21.
21Kisha Isiraeli akamwambia Yosefu: Tazama! Mimi ninakufa, lakini Mungu atakuwa pamoja nanyi, awarudishe katika nchi ya baba zenu. 22Nami nimekupa fungu moja zaidi ya ndugu zako, nililolichukua kwao Waamori kwa upanga wangu na kwa upindi wangu.#Yoh. 4:5.

Iliyochaguliwa sasa

1 Mose 48: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia