Yohana 14
14
Kwenda kwa Baba.
1Mioyo yenu isizizimke! Mtegemeeni Mungu, nami mnitegemee! 2Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi. Kama visingekuwa hivyo, ningewaambia: Nakwenda kuwatengenezea mahali. 3Nami ijapokuwa ninakwenda kuwatengenezea mahali, nitakuja tena, niwachukue kuwapeleka mwangu, kwamba nanyi mwepo hapo, nilipo mimi.#Yoh. 12:26; 17:24. 4Nayo njia ya kwenda pale, nitakapokwenda mimi, mmeijua. 5Ndipo, Toma alipomwambia: Bwana, tusipopajua, unapokwenda, njia tutaijuaje? 6Yesu akamwambia: Mimi ndiyo njia na kweli na uzima; hakuna atakayefika kwa Baba asiponishika mimi.*#Yoh. 11:25; Mat. 11:27; Rom. 5:1-2; Ebr. 10:20. 7Kama mngenitambua mimi, mngemjua hata Baba yangu. Tangu sasa mwamtambua, tena mmemwona. 8Filipo akamwambia: Bwana, tuonyeshe Baba! hivi vitatutosha. 9Yesu akamwambia: Miaka hii yote nipo pamoja nanyi, nawe hujanitambua, Filipo? Aliyeniona mimi amekwisha kumwona Baba. Unasemaje: Tuonyeshe Baba?#Yoh. 12:45; Ebr. 1:3. 10Huyategemei, ya kuwa mimi nimo mwa Baba, naye Baba yumo mwangu mimi? Maneno, ninayowaambia, siyasemi kwa mawazo yangu mwenyewe, ila Baba anayekaa mwangu ndiye anayezitenda kazi zake.#Yoh. 12:49. 11Nitegemeeni, ya kuwa mimi nimo mwake Baba, naye Baba yumo mwangu mimi! Lakini mkishindwa, nitegemeeni kwa ajili ya kazi zizo hizo!#Yoh. 10:25,38; 14:20. 12Kweli kweli nawaambiani: Mwenye kunitegemea naye yeye atazifanya kazi, ninazozifanya mimi, naye atafanya zilizo kubwa kuliko hizi, maana mimi nakwenda kwa Baba.#Mar. 16:19-20. 13Tena lo lote, mtakaloliomba katika Jina langu, nitalifanya, Baba apate kutukuzwa, kwa kuwa yumo mwake Mwana.#Yoh. 15:7; Mar. 11:24. 14Mtakaloniomba katika Jina langu, nitalifanya.#Yoh. 16:23-24; 1 Yoh. 5:14-15.
Kiagio cha Roho Mtakatifu.
15*Mkinipenda yashikeni maagizo yangu! 16Nami nitamwomba Baba, naye atawapa mtuliza mioyo mwingine, akae pamoja nanyi kale na kale.#Yoh. 15:10; 1 Yoh. 5:3. 17Ndiye Roho wa kweli, ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni, wala haumtambui. Ninyi mnamtambua, kwani anakaa kwenu, naye atakuwamo mwenu.#Yoh. 14:26; 15:26; 16:7; Yes. 51:12. 18Sitawaacha peke yenu, nitakuja kwenu.#Yoh. 16:13; 7:39. 19Bado kidogo ulimwengu hautaniona tena, lakini ninyi mtaniona, kwani mimi nipo ninaishi, nanyi mtakuwa mnaishi.#Yoh. 16:16; 20:20. 20Siku ile mtatambua ninyi, ya kuwa mimi nimo mwake Baba yangu, nanyi mmo mwangu, nami nimo mwenu.#Yoh. 17:21-23. 21Aliye na maagizo yangu, akiyashika, huyo ndiye mwenye kunipenda. Lakini mwenye kunipenda atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda nimwonyeshe, nilivyo.*#2 Kor. 3:18. 22Yuda, lakini siye Iskariota, akamwambia: Bwana, imekuwaje, ukitaka kutuonyesha sisi, ulivyo, usipovionyesha wao wa ulimwengu?#Tume. 10:40-41.
23*Yesu akajibu, akamwambia: Mtu akinipenda atalishika Neno langu, naye Baba yangu atampenda, nasi tutamfikia, tufanye makao kwake.#Yoh. 13:34; 14:21; Fano. 8:17; Ef. 3:17. 24Asiyenipenda hayashiki maneno yangu; nalo Neno, mnalolisikia, silo langu, ila la Baba aliyenituma.#Yoh. 7:16.
25Haya nimewaambia nikingali kwenu. 26Lakini yule mtuliza mioyo, yule Roho Mtakatifu, Baba atakayemtuma katika Jina langu, ndiye atakayewafundisha yote na kuwakumbusha yote, mimi niliyowaambia ninyi.#Yoh. 14:16. 27Nawaachia utengemano, utengemano wangu nawapani. Mimi siwapi, kama ulimwengu unavyowapa. Mioyo yenu isizizimke, wala isiogope!#Yoh. 16:33; Fil. 4:7. 28Mmesikia, nilivyowaambia: Nakwenda zangu, tena nitawajia. Kama mngenipenda, mngefurahi, ya kuwa nakwenda kwa Baba, kwani Baba ni mkubwa kuliko mimi.#Yoh. 14:3,6,18. 29Sasa nimewaambia, yanapokuwa hayajafanyika bado, mpate kunitegemea, yatakapofanyika. 30Sitasema nanyi mengi tena, kwani mtawala ulimwengu huu anakuja; lakini hakuna tena, anachokiweza kwangu mimi,#Yoh. 12:31; Ef. 2:2. 31ni kwamba tu, ulimwengu upate kutambua, ya kuwa nampenda Baba, nikafanya hivyo, Baba alivyoniagiza., Inukeni, tutoke humu!*#Yoh. 10:18.
Iliyochaguliwa sasa
Yohana 14: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.