Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohana 13

13
Kuwaosha miguu.
1*Sikukuu ya Pasaka ilipokuwa haijatimia, Yesu alikuwa amejua, ya kuwa saa yake imefika, autoke ulimwengu huu, aende kwa Baba; kwa kuwa aliwapenda watu wake waliomo ulimwenguni, akawapenda mpaka mwisho. 2Walipokula chakula cha jioni, Msengenyaji alikuwa amekwisha kutia moyoni mwa Yuda wa Simoni Iskariota mawazo ya kumchongea.#Luk. 22:3. 3Kwa hivyo, Yesu alivyojua, ya kuwa Baba alimpa yote mikononi mwake, ya kuwa alitoka kwa Mungu, tena anarudi kwa Mungu,#Yoh. 3:35; 16:28. 4akainuka penye chakula, akaivua kanzu yake, akatwaa kitambaa cha ukonge, akajifunga kiunoni. 5Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwaosha wanafunzi miguu na kuisugua kwa kile kitambaa, alichojifunga kiunoni. 6Alipomfikia Simoni Petero, akamwambia; Bwana, wewe unioshe miguu? 7Yesu akajibu, akamwambia: Ninachokifanya mimi, wewe hukijui sasa, lakini utakitambua halafu. 8Petero alipomwambia: Hutaniosha miguu kale na kale, Yesu akamjibu: Nisipokuosha, hakuna fungu lako tena lililoko kwangu. 9Ndipo, Simoni Petero alipomwambia: Bwana, usinioshe miguu tu, nioshe hata mikono na kichwa! 10Yesu akamwambia: Aliyekwisha koga harudi tena kunawa, isipokuwa miguu, kwani ametakata wote. Nanyi mmetakata, lakini sio wote.#Yoh. 15:3. 11Kwani alimjua mwenye kumchongea; kwa hiyo alisema: Hamtakati nyote.#Yoh. 6:64,70-71.
Chakula cha Pasaka.
12Alipokwisha kuwaosha miguu akayatwaa mavazi yake, akakaa tena chakulani, akawaambia; Mwakitambua, nilichowafanyia? 13Ninyi mnaniita Mfunzi na Bwana, mnasema vema hivyo, kwani ndimi.#Mat. 23:8,10. 14Basi, mimi niliye Bwana na Mfunzi wenu nikiwaosha ninyi miguu, imewapasa nanyi kuoshana miguu.#Luk. 22:27. 15Kwani nimewapani la kujifunziamo, mfanyiane ninyi kwa ninyi, kama nilivyowafanyia mimi.*#Fil. 2:5; Kol. 3:13. 16Kweli kweli nawaambiani: Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake, wala mjumbe si mkubwa kuliko yule aliyemtuma.#Mat. 10:24. 17Mkiyajua haya m wenye shangwe mkiyafanya.#Mat. 7:24. 18Siyasemi ya ninyi nyote; mimi nawajua, niliowachagua. Lakini sharti andiko litimizwe la kwamba:
Anayeula mkate wangu hunipiga mateke.#Sh. 41:10. 19Nawaambia haya sasa, yanapokuwa hayajafanyika bado, kusudi hapo, yatakapofanyika, mpate kuyategemea, ya kuwa mimi ndiye. 20Kweli kweli nawaambiani: Atakayempokea ye yote, nitakayemtuma, hunipokea mimi; naye mwenye kunipokea mimi humpokea aliyenituma.#Mat. 10:40.
Kumjulisha Yuda.
(21-30: Mat. 26:21-25; Mar. 14:18-21; Luk. 22:21-23.)
21Yesu alipokwisha kuyasema haya akazizimka jrohoni, akawashuhudia akisema: Kweli kweli nawaambiani: Mwenzenu mmoja atanichongea.#Yoh. 12:27. 22Wanafunzi wakatazamana, maana hawakumjua, aliyemsema. 23Palikuwapo mwanafunzi wake mmoja aliyeegamia kifuani pa Yesu, ndiye, Yesu aliyempenda.#Yoh. 19:26; 20:2; 21:20. 24Simoni Petero akamkonyeza huyo, amwulize, kama ni nani, anayemsema. 25Kisha yule aliyemwegamia Yesu kifuani akamwuliza: Bwana, ni nani? 26Yesu akajibu: Ni yule, mimi nitakayemtowelea kitonge na kumpa. Basi, akatowelea kitonge, akakitwaa, akampa Yuda wa Simoni Iskariota. 27Alipokwisha kukila kile kitonge, ndipo, Satani alipomwingia. Yesu akamwambia: Utakachokifanya, kifanye upesi!#Yoh. 13:2; Luk. 22:3. 28Lakini wale waliokaa chakulani hakuna aliyeitambua sababu ya kumwambia hivyo; 29wengine wakawaza: kwa sababu Yuda aliushika mfuko wa senti, Yesu alimwambia: Nunua chakula cha siku za sikukuu! au agawie maskini kidogo.#Yoh. 12:6. 30Basi, yeye alipokwisha kukipokea kile kitonge akatoka nje papo hapo, lakini ulikuwa usiku.
Agizo jipya.
31*Yule alipokwisha toka, Yesu akasema: Sasa Mwana wa mtu ametukuzwa, naye Mungu ndiye aliyetukuzwa kwake.#Yoh. 12:28. 32Kama Mungu alitukuzwa kwake, yeye Mungu atamtukuza kwake mwenyewe, tena atamtukuza upesi.#Yoh. 12:23; 17:1-5. 33Vitoto, nipo pamoja nanyi bado kidogo; kisha mtanitafuta, lakini kama nilivyowaambia Wayuda: Ninyi hamwezi kupafika pale, ninapokwenda mimi, ndivyo, ninavyowaambia hata ninyi sasa.#Yoh. 8:21. 34Nawapa agizo jipya: Mpendane! Kama nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo!#Yoh. 15:12-13,17. 35Kwa hiyo wote watatambua, ya kama m wanafunzi wangu mimi, mtakapopendana ninyi kwa ninyi.*
Kumwonya Petero
(36-38: Mat. 26:33-35; Mar. 14:29-31; Luk. 22:31-34.)
36Simoni Petero akamwambia: Bwana, unakwenda wapi? Yesu akajibu: Pale ninapokwenda, huwezi kunifuata sasa, lakini utanifuata halafu.#Yoh. 7:34; 21:18-19. 37Petero akamwambia: Bwana, kwa nini siwezi sasa kufuatana na wewe? 38Hata roho yangu nitaitoa kwa ajili yako wewe.#Mat. 26:34. 39Yesu akajibu: Uitoe roho yako kwa ajili yangu mimi? Kweli kweli nakuambia: Jogoo hatawika, usipokuwa umekwisha kunikana mara tatu.

Iliyochaguliwa sasa

Yohana 13: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia