Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohana 12

12
Yesu anamiminiwa mafuta.
(1-8: Mat. 26:6-13; Mar. 14:3-9.)
1Siku sita mbele ya kuwa Pasaka Yesu akaenda Betania, ndiko kwao Lazaro, Yesu aliyemfufua katika wafu.#Yoh. 11:1,43. 2Kule wakamwandalia chakula cha jioni, naye Marta alikuwa akiwatumikia; lakini Lazaro alikuwa mmoja wao waliokaa chakulani naye. 3Ndipo, Maria alipoleta kichupa cha mafuta ya maua yanayoitwa Narada, ni yenye bei kubwa, nayo yalikuwa hayakuchanganywa na mengine. Akampaka Yesu miguu, kisha akaisugua miguu yake kwa nywele zake; namo nyumbani mote pia mkanukia hayo mafuta ya maua.#Luk. 7:38. 4Yuda Iskariota, mmoja wao wanafunzi wake, ndiye aliyemchongea halafu, akasema: 5Kwa sababu gani mafuta haya hayakuuzwa kwa shilingi 300, wakapewa maskini? 6Lakini akisema hivyo, si kwa sababu ya kutunza maskini, ila kwa sababu ya kuwa mwizi; naye ndiye aliyeushika mfuko akivichukua, walivyopewa.#Luk. 8:3. 7Yesu akasema: Umwache! Maana alikuwa ameyawekea siku ya kuzikwa kwangu. 8Kwani maskini mnao kwenu siku zote, lakini mimi hamwi nami siku zote.*#5 Mose 15:11.
Njama ya kumwua Lazaro.
9Kundi la Wayuda wengi walipotambua, ya kuwa yuko kule, wakaja, si kwa ajili ya Yesu tu, ila walitaka kumwona naye Lazaro, aliyemfufua katika wafu. 10Kwa hiyo watambikaji wakuu wakala njama ya kumwua hata Lazaro. 11Kwani kwa ajili yake yeye Wayuda wengi wakaenda kule, wakamtegemea Yesu.
Kuingia Yerusalemu.
(12-19: Mat. 21:1-11; Mar. 11:1-10; Luk. 19:29-40.)
12*Kesho yake wale watu wengi walioijia sikukuu waliposikia, ya kuwa Yesu anakuja Yerusalemu, 13wakachukua makuti ya mitende, wakatoka kumwendea, wakapaza sauti:
Hosiana! Na atukuzwe ajaye kwa Jina la Bwana!
Ndiye mfalme wa Isiraeli!#Sh. 118:25,26. 14Yesu alipoona kipunda akampanda, kama ilivyoandikwa:
# Zak. 9:9. 15Usiogope, binti Sioni! Tazama, mfalme wako anakuja,
amepanda mwana wa punda!
16Hayo wanafunzi wake kwanza hawakuyatambua, ila Yesu alipokwisha kuupata utukufu wake, ndipo, walipokumbuka, ya kuwa aliandikiwa hayo, tena ndiyo, waliyomfanyizia. 17Hata wale watu wengi waliokuwa pamoja naye, alipomfufua Lazaro katika wafu na kumwita, atoke kaburini, wakavishuhudia. 18Kwa sababu hiyo watu wengi wakamwendea, kwani walikuwa wamesikia, ya kuwa yeye amekifanya kielekezo hicho.* 19Mafariseo wakasemezana wao kwa wao: Tazameni, hakuna mnayoyaweza! Tazameni, watu wote pia wamekwenda kumfuata!#Yoh. 11:48.
Wagriki wanamwendea Yesu.
20*Miongoni mwao waliopanda kutambika siku za ile sikukuu mlikuwa na Wagriki. 21Hao wakamjia Filipo wa Beti-Saida wa Galilea, wakambembeleza wakisema: Bwana, twataka kumwona Yesu.#Yoh. 1:44. 22Filipo akaenda, akamwambia Anderea. Anderea na Filipo wakaenda, wakamwambia Yesu. 23Ndipo, Yesu alipowajibu akisema: Saa imefika, Mwana wa mtu atukuzwe. 24Kweli kweli nawaambia: Punje ya ngano isipoanguka mchangani kufia mle, hukaa peke yake yenyewe tu; lakini inapokufa huleta mbegu nyingi.#Rom. 14:9; 1 Kor. 15:36. 25Mwenye kuipenda roho yake huiangamiza; naye mwenye kuichukia roho yake humu ulimwenguni ataiponya, aifikishe penye uzima wa kale na kale.#Mat. 10:39; Luk. 17:33. 26Mtu akinitumikia, sharti anifuate mimi; napo hapo, nilipo mimi, papo hapo hata mtumishi wangu sharti awepo. Mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.*#Yoh. 14:3; 17:24. 27Sasa roho yangu imezizimka, nami nisemeje? Niseme: Baba, uniokoe, nisiifikie saa hiyo? Lakini kwa sababu hiyo nimeijia saa hiyo.#Mat. 26:38. 28Basi, niseme: Baba, ulitukuze Jina lako! Kisha sauti ikaja toka mbinguni kwamba: Nimelitukuza, kisha nitalitukuza tena.#Yoh. 13:31; 17:4-5. 29Kundi la watu waliokuwako walipoyasikia wakasema: Kumepiga ngurumo; wengine wakasema: Malaika amesema naye. 30Yesu akajibu akisema: Sauti hii haikutoka kwa ajili yangu, ila kwa ajili yenu.#Yoh. 11:42. 31Sasa hukumu ya ulimwengu imetimia; hivi sasa mtawala ulimwengu huu atasukumwa, autoke.#Yoh. 14:30; 16:11; Luk. 10:18. 32Mimi nitakapokwezwa, nitoke nchini, ndipo, nitakapowavuta wote, waje kwangu.#Yoh. 8:28. 33Neno hili alilisema, aonyeshe, kama ni kufa gani kulikomngoja. 34Watu wakamjibu: Sisi tumesikia katika Maonyo: Kristo atakaa kale na kale; tena inakuwaje, wewe ukisema: Mwana wa mtu sharti akwezwe juu? Huyo Mwana wa mtu ni nani?#Sh. 110:4; Dan. 7:14. 35Yesu akawaambia: Mwanga ungaliko kwenu siku chache. Fanyeni mwendo mnapokuwa mnao mwanga, giza isiwaguie!#Yoh. 8:12; 11:10. 36Anayejiendea gizani hajui, anakokwenda. Mkiwa mnao mwanga utegemeeni mwanga, mpate kuwa wana wa mwanga!#Ef. 5:9.
Wapenzi na wachukivu wa Yesu.
37Yesu alipokwisha kuyasema haya, akaenda zake, akajificha, wasimwone tena. Lakini ijapokuwa amefanya mbele yao vielekezo vingi kama hivyo, hawakumtegemea. 38Imekuwa hivyo, neno, mfumbuaji Yesaya alilolisema, lipate kutimia:
Bwana, yuko nani anayeutegemea utume wetu?
Tena yuko nani aliyefumbuliwa, mkono wa Bwana
unayoyafanya?#Yes. 53:1; Rom. 10:16. 39Kwa sababu hii hawakuweza kumtegemea, kwani Yesaya alisema tena:#Yes. 6:9-10; Mat. 13:14-15.
40Amewapofua macho, akaishupaza mioyo yao,
wasije wakaona kwa macho yao, au wakajua maana kwa mioyo
yao, au wakageuka, nami nikawaponya.
41Yesaya aliyasema hayo, kwani aliuona utukufu wake, akayasema mambo yake yeye.#Yes. 6:1. 42Vivyo hivyo hata katika wakubwa walikuwamo wengi waliomtegemea, lakini kwa ajili ya Mafariseo hawakuungama, wasikatazwe kuiingia nyumba ya kuombea.#Yoh. 9:22. 43Kwani kutukuzwa na watu walikupenda kuliko kutukuzwa na Mungu.#Yoh. 5:44.
Mungu amemtuma Yesu.
44Lakini Yesu alipaza sauti, akasema: Anayenitegemea hanitegemei mimi, ila humtegemea yule aliyenituma. 45Tena, anayeniona mimi humwona yule aliyenituma.#Yoh. 14:9. 46Mimi nimekuja ulimwenguni kuwa mwanga, kila anitegemeaye asikae gizani.#Yoh. 12:35. 47Mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu. Kwani sikujia kuuhukumu ulimwengu, ila nimejia kuuokoa ulimwengu.#Yoh. 3:17; Luk. 9:56. 48Anikataaye, asiyapokee maneno yangu, anaye atakayemhukumu. Neno, nililolisema, ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho. 49Kwani mimi sikuyasema maneno yangu, ila Baba mwenyewe aliyenituma ameniagiza, nitakayoyasema na kuyafundisha. 50Nami nayajua, aliyoyaagiza, ya kuwa ni uzima wa kale na kale. Basi, ninayoyasema, ninayasema, kama Baba alivyoniambia.

Iliyochaguliwa sasa

Yohana 12: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia