Yohana 11
11
Kufa kwake Lazaro.
1*Kulikuwa na mtu mgonjwa, ndiye Lazaro wa Betania, ni kijiji chao Maria na ndugu yake Marta;#Luk. 10:38-39. 2Maria ndiye yule aliyempaka Bwana mafuta na kuisugua miguu yake kwa nywele zake. Huyo umbu lake Lazaro alikuwa mgonjwa.#Yoh. 12:3. 3Dada zake wakatuma kwake kwamba: Bwana, tazama, unayempenda ni mgonjwa! 4Yesu alipovisikia akasema: Ugonjwa huu sio wa kufa, ni wa kuuonyesha utukufu wake Mungu, Mwana wa Mungu apate kutukuzwa nao.#Yoh. 9:3; 11:40. 5Lakini Yesu alikuwa amewapenda akina Marta na ndugu yake na Lazaro. 6Aliposikia, ya kuwa ni mgonjwa, akakaa siku mbili hapo, alipokuwapo. 7Kisha ndipo, alipowaambia wanafunzi: Twende Yudea tena! 8Wanafunzi walipomwambia: Mfunzi mkuu, sasa hivi Wayuda walitafuta kukupiga mawe, nawe unarudi huko tena?#Yoh. 8:59; 10:31. 9Yesu akajibu: Saa za mchana sizo kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai, kwani huuona mwanga wa ulimwengu huu;#Yoh. 9:4-5. 10lakini mtu akienda usiku hujikwaa, kwani mwanga haumo mwake.#Yoh. 12:35. 11Alipokwisha kusema hivyo akawaambia: Mpenzi wetu Lazaro amelala, lakini nakwenda, nimwamshe.*#Mat. 9:24. 12Wanafunzi wakamwambia: Bwana, akiwa amelala atapona. 13Lakini Yesu alikuwa amesema kufa kwake, lakini wale walidhani: alisema kulala usingizi. 14Ndipo, Yesu alipowaambia waziwazi: Lazaro amekufa. 15Nami nafurahi kwa ajili yenu, ya kuwa sikuwako kule, mpate kunitegemea. Lakini twende, tufike kwake! 16Toma anayeitwa Pacha akawaambia wanafunzi wenziwe: Twende nasi, tufe pamoja naye!
17Yesu alipokuja akamkuta, amekwisha kuwa kaburini siku nne. 18Lakini kule Betania kulikuwa karibu ya Yerusalemu, ni mwendo wa nusu saa; 19kwa hiyo Wayuda wengi walikuwa wamekuja kwao Marta na Maria, wawatulize mioyo kwa ajili ya umbu lao.
20*Marta aliposikia, ya kuwa Yesu anakuja, akaenda kumkuta njiani; lakini Maria alikuwa akikaa nyumbani. 21Marta akamwambia Yesu: Bwana, kama ungalikuwapo hapa, umbu langu hangalikufa. 22Lakini na sasa najua, ya kuwa yote, utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa. 23Yesu alipomwambia: Umbu lako atafufuka,#Yoh. 5:28-29; 6:40; Mat. 22:23-33; Luk. 14:14. 24Marta akamwambia: Najua, ya kuwa atafufuka, wafu watakapofufuka siku ya mwisho. 25Yesu akamwambia: Mimi ndio ufufuko na uzima; anitegemeaye atapata uzima, ajapokufa. 26Kila aliye mzima na kunitegemea hatakufa kale na kale. Unavitegemea hivi?#Yoh. 8:51. 27Akamwambia: Ndio, Bwana, mimi nimeyategemea, ya kuwa wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, anayekuja ulimwenguni.*#Yoh. 6:69.
Kumfufua Lazaro.
28Alipokwisha kusema hivyo akaondoka, akamwita ndugu yake Maria na kufichaficha, akasema: Mfunzi yuko, anakwita. 29Naye alipovisikia akainuka upesi, akamwendea; 30maana Yesu alikuwa hajaingia kijijini, ila alikuwa bado hapo, Marta alipomkuta.#Yoh. 11:20. 31Wayuda waliokuwa pamoja naye nyumbani na kumtuliza moyo walipomwona Maria, alivyoinuka upesi na kutoka, wakamfuata wakiwaza, ya kuwa anajiendea kaburini, alie huko. 32Maria alipofika hapo, Yesu alipokuwa, akamwangukia miguuni alipokwisha kumwona, akamwambia: Bwana, kama ungalikuwapo hapa, umbu langu hangalikufa. 33Yesu alipoona, anavyolia, nao Wayuda waliokuja pamoja naye wanavyolia nao, akachemka rohoni, akajisisimua,#Yoh. 13:21. 34akauliza: Mmemzika wapi? Wakamwambia: Njoo, Bwana, utazame! 35Naye Yesu machozi yakamtoka.#Luk. 19:41. 36Ndipo, Wayuda waliposema: Tazameni, alivyompenda! 37Lakini wengine wao wakasema: Huyu aliyemfumbua kipofu macho hakuweza kuzuia, huyu naye asife? 38Yesu akachemka tena moyoni, akafika penye kaburi; hilo lilikuwa pango lenye jiwe lililowekwa mlangoni pake.#Mat. 27:60. 39Yesu aliposema: Liondoeni hili jiwe! Marta, dada yake aliyekufa, akamwambia: Bwana, ameanza kunuka, kwani leo ni siku ya nne. 40Yesu akamwambia: Sikukuambia: Ukinitegemea utauona utukufu wake Mungu?#Yoh. 4:23,25-26. 41Basi, wakaliondoa jiwe. Kisha Yesu akayaelekeza macho juu, akasema: Baba, nakushukuru, ya kuwa umenisikia. 42Mimi nimekujua, ya kuwa unanisikia po pote; lakini kwa ajili ya kundi la watu wanaosimama hapa ninasema hivyo, wapate kuyategemea, ya kuwa wewe umenituma.#Yoh. 12:30. 43Alipokwisha kuyasema haya akaita na kupaza sauti: Lazaro, toka nje! 44Ndipo, yule aliyekufa alipotoka nje hivyo, alivyokuwa amefungwa kwa sanda miguu na mikono, nao uso wake ulikuwa umefunikwa kwa mharuma. Yesu akawaambia: Mfungueni, mmwache, aende zake!
Njama ya kumwua Yesu.
45Wayuda wengi waliomjia Maria walipoliona, alilolifanya, wakamtegemea, 46lakini wengine wao wakaenda zao kwa Mafariseo, wakawaambia, Yesu aliyoyafanya.
47*Ndipo, watambikaji wakuu na Mafariseo walipoikusanya baraza ya wakuu wote, wakasema: Tufanyeje? Kwani mtu huyu anafanya vielekezo vingi. 48Tukimwacha hivyo, wote watamtegemea, kisha Waroma watakuja, waichukue nchi yetu pamoja na watu wetu. 49Lakini mwenzao Kayafa aliyekuwa mtambikaji mkuu wa mwaka ule akawaambia: Ninyi hamjui kitu, 50wala hamfikiri, ya kuwa inawafalia ninyi, mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, kabila lote lisiangamie.#Yoh. 18:14. 51Lakini neno hili hakulisema kwa mawazo yake, ila kwa kuwa alikuwa mtambikaji mkuu wa mwaka ule, alifumbua yajayo, kwani Yesu alitumwa afe kwa ajili ya kabila lote;#2 Mose 8:30; 4 Mose 7:21. 52lakini siko kufa kwa ajili ya kabila lake tu, ila ni kwamba, apate kuwakusanya pamoja nao watoto wa Mungu waliotawanyika.#Yoh. 10:16. 53Basi, tangu siku ile walikula njama ya kumwua.
54Naye Yesu hakutembea tena waziwazi kwa Wayuda, ila akaondoka kule, akaenda katika nchi iliyokuwa karibu ya nyikani, akaingia mji uitwao Efuraimu. Mle akakaa pamoja na wanafunzi. 55Lakini Pasaka ya Wayuda ilikuwa karibu; kwa hiyo wengi wa nchi ile wakapanda kwenda Yerusalemu, Pasaka ilipokuwa bado, wapate kujieua.#2 Mambo 30:17. 56Kwa kumtafuta Yesu wakasemezana wao kwa wao wakisimama hapo Patakatifu: Mwaonaje? Hatakuja sikukuu hii? 57Lakini watambikaji wakuu na Mafariseo walikuwa wameagiza, mtu akitambua, alipo, sharti aseme, wapate kumkamata.*
Iliyochaguliwa sasa
Yohana 11: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.