Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohana 10

10
Mchungaji mwema.
1Kweli kweli nawaambiani: Asiyepita mlangoni, apate kuingia zizini mwa kondoo, akipandia pengine, huyo ni mwizi na mnyang'anyi. 2Lakini anayeingia mlangoni ndiye mchungaji wa kondoo. 3Mlinda mlango anamfungulia huyo, nao kondoo humsikia sauti yake. Naye huwaita kondoo walio wake kwa majina yao, huwatoa nje. 4Akiisha kuwatoa nje hutangulia mbele yao wote walio wake, nao kondoo humfuata, kwani wameijua sauti yake. 5Lakini mgeni hawatamfuata, ila watamkimbia, kwani hawazijui sauti za wageni. 6Fumbo hili Yesu aliwaambia, lakini wale hawakuitambua maana yao, aliyowaambia.
7Yesu akasema tena: Kweli kweli nawaambiani: Mimi ndio mlango wa kondoo. 8Wo wote waliokuja mbele yangu ndio wezi na wanyang'anyi; kwa hiyo kondoo hawakuwasikia.#Yer. 23:1-2. 9Mimi ndio mlango. Mtu akiingilia kwangu mimi ataokoka, atakapoingia napo atakapotoka, apate malisho. 10Mwizi haji, asipotaka kwiba na kuchinja na kuangamiza. Mimi nimekuja, wakae wenye uzima na wenye vingine vyote.
11*Mimi ndiye mchungaji mwema; mchungaji mwema hujitoa kwa ajili ya kondoo.#Sh. 23:1. 12Lakini mfanya kazi, asiye mchungaji wala mwenye kondoo, huwaacha kondoo na kukimbia anapomwona chui, akija. Naye chui huwakamata na kuwatawanya.#Yoh. 15:13; Yes. 40:11; Ez. 34:11-23; 37:24. 13Kwani yeye ni mfanya kazi tu, hawasumbukii kondoo. 14Mimi ndiye mchungaji mwema, ninawatambua walio wangu, nao walio wangu hunitambua mimi;#2 Tim. 2:19. 15ndivyo, kama Baba anavyonitambua mimi, na kama mimi ninavyomtambua Baba. Nami mwenyewe ninajitoa, nife kwa ajili ya kondoo.#Mat. 11:27. 16tena ninao kondoo wengine, wasio wa zizi hili; nao hao sharti niwalete, nao wataisikia sauti yangu; kisha watakuwa kundi moja na mchungaji mmoja.*#Yoh. 11:52; Tume. 10:34-35. 17Kwa hiyo Baba ananipenda, kwa sababu najitoa mwenyewe, nife, nipate tena kuwapo. 18Hakuna anayenishurutisha hivyo, ila mimi ninajitoa mwenyewe. Nina uwezo wa kujitoa, nife, tena nina uwezo wa kuwapo tena. Hivi ndivyo, alivyoniagiza Baba yangu.#Yoh. 5:26.
19Wayuda wakakosana tena kwa ajili ya maneno haya.#Yoh. 7:43; 9:16. 20Wengine wao wakasema: Ana pepo, tena yuko na wazimu. Mwamsikilizaje?#Yoh. 7:20. 21Wengine wakasema: Maneno haya siyo ya mwenye wazimu. Yuko pepo awezaye kuwafumbua vipofu macho?
Yesu na Baba ni mmoja.
22Kisha pakawa na sikukuu ya mweuo wa Patakatifu huko Yerusalemu; siku zake zilikuwa za kipupwe.
23*Yesu alipokuwa anatembea hapo Patakatifu katika ukumbi wa Salomo,#Tume. 3:11. 24Wayuda wakamzunguka, wakamwambia: Unatuhangisha roho zetu mpaka lini? Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie waziwazi! 25Yesu akawajibu: Naliwaambia, nanyi hamnitegemei. Kazi, ninazozifanya katika Jina la Baba yangu, hizo zinanishuhudia.#Yoh. 5:36. 26Lakini ninyi hamnitegemei, kwani ninyi hammo katika kondoo wangu.#Yoh. 8:45. 27Kondoo wangu huisikia sauti yangu, nami nawajua, nao hunifuata.#Yoh. 8:47; 10:3-4. 28Nami nawapa uzima wa kale na kale; hawataangamia kale na kale, wala hakuna mtu atakayewapoka mkononi mwangu. 29Yeye Baba aliyenipa wale ni mkubwa kuliko wote; hakuna mtu anayeweza kuwapoka mkononi mwake Baba. 30Mimi na Baba tu mmoja.* 31Wayuda walipookota tena mawe, wamtupie,#Yoh. 8:59. 32Yesu akawajibu: Matendo mengi yaliyo mazuri nimewaonyesha kwa nguvu ya Baba; katika hayo ni lipi, mwatakalo kunipigia mawe? 33Wayuda wakamjibu: Si kwa ajili ya tendo zuri, tukitaka kukupiga mawe, ila kwa ajili ya kumbeza Mungu, kwani wewe uliye mtu unajifanya kuwa Mungu.#Yoh. 5:18; Mat. 9:3; 26:65. 34Yesu akawajibu: Katika Maonyo yenu hamkuandikwa kwamba: Mimi nalisema: Ninyi m miungu? Nalo lililoandikwa haliwezi kutanguliwa.#Sh. 82:6. 35Kama aliwaita wale miungu walioambiwa Neno la Mungu, 36basi, mimi, ambaye Baba alinitakasa na kunituma ulimwenguni, mwanisemaje: Unambeza Mungu, kwa sababu nalisema: Mimi ni Mwana wake Mungu?#Yoh. 5:17-20. 37Nisipoyafanya matendo ya Baba yangu, msinitegemee! 38Lakini ninapoyafanya, yategemeeni matendo hayo, msipotaka kunitegemea mimi! Nanyi mpate kujua na kutambua, ya kuwa Baba yumo mwangu, nami nimo mwake Baba. 39Basi, wakatafuta tena kumkamata, lakini akatoka mikononi mwao.#Yoh. 8:59; Luk. 4:30.
40Kisha akaondoka tena kwenda ng'ambo ya Yordani mahali pale, Yohana alipokuwa akibatiza hapo kwanza; akakaa pale.#Yoh. 1:28. 41Watu wengi wakamwendea hapo, wakasema: Yohana hakufanya kielekezo cho chote, lakini yote, Yohana aliyoyasema yake huyu, yalikuwa ya kweli. 42Kwa hiyo wengi wakamtegemea pale.

Iliyochaguliwa sasa

Yohana 10: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia