Yohana 9
9
Mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa.
1Alipokuwa akitambea akaona amtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa.#Luk. 13:2. 2Wanafunzi wakamwuliza wakisema: Mfunzi mkuu, aliyekosa ni nani? Huyu au wazazi wake, akizaliwa kipofu? 3Yesu akajibu: Hawakukosa wala huyu wala wazazi wake, ila alizaliwa hivyo, kazi ya Mungu ionekane kwake.#Yoh. 11:4. 4Sisi sharti tuzifanye kazi zake aliyenituma, mchana ukingali upo. Usiku unakuja, pasipowezekana kufanya kazi.#Yoh. 5:17. 5Nikingali ulimwenguni, mimi ndio mwanga wa ulimwengu.#Yoh. 8:12. 6Alipokwisha kuyasema haya akatena mate chini, akayavuruga hayo mate kuwa kitope, nacho kitope akampaka machoni,#Mar. 8:23. 7akamwambia: Nenda, unawe katika ziwa la Siloa, ni kwamba: Aliyetumwa. Basi, akaenda, akanawa, akarudi mwenye kuona.#Yes. 8:6.
8Majirani zake nao waliomwona siku zote, alivyokaa na kuombaomba, wakasema: Huyu siye aliyekuwa amekaa na kuombaomba? 9Wengine wakasema: Ndiye; wengine wakasema: Siye, wamefanana tu; yeye akasema: Mimi ndiye. 10Basi, wakamwuliza: Macho yako yamefumbukaje? 11Akajibu: Yule mtu anayeitwa Yesu alivuruga kitope, akanipaka machoni, akaniambia: Uende penye ziwa la Siloa, unawe! Nikaenda, nikanawa, nikapata kuona. 12Walipomwuliza: Yuko wapi huyo? akasema: Sijui.
13Wakampeleka kwa Mafariseo yule aliyekuwa ni kipofu. 14Lakini siku, Yesu alipokivuruga kitope na kumfumbua macho yake, ilikuwa ya mapumziko.#Yoh. 5:9. 15Mafariseo walipomwuliza tena, alivyopata kuona, akawaambia: Alinipaka kitope machoni, nikanawa, ndio naona. 16Kwao Mafariseo walikuwako waliosema: Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwani haishiki miiko ya siku ya mapumziko. Wengine waliposema: Mtu mkosaji awezaje kuvifanya vielekezo kama hivyo? wakakosana wao kwa wao.#Yoh. 7:43; 9:31,33. 17Kwa hiyo wakamwambia kipofu tena: Wewe unamwona kuwa nani, kwa sababu alikufumbua macho? Naye akasema: Ni mfumbuaji. 18Basi, Wayuda hawakulisadiki neno lake, ya kuwa alikuwa ni kipofu, akapata kuona, mpaka walipowaita wazazi wake yeye aliyepata kuona; 19wakawauliza: Huyu ndiye mwana wenu, mnayemsema: Alizaliwa kipofu? Sasa amepataje kuona? 20Wazazi wake wakajibu, wakasema: Twajua, huyu ni mwana wetu, naye alizaliwa kipofu; 21lakini hatujui, jinsi alivyopata kuona sasa, wala hatumjui sisi aliyemfumbua macho. Mwulizeni mwenyewe! Ni mtu mzima; atajisemea mwenyewe. 22Wazazi wake walisema hivyo kwa kuwaogopa Wayuda, kwani Wayuda walikuwa wamekula njama ya kwamba: Mtu atakayemwungama, kuwa ni Kristo, akatazwe kuiingia nyumba ya kuombea.#Yoh. 7:13; 12:42. 23Kwa hiyo wazazi wake walisema: Ni mtu mzima, mwulizeni mwenyewe!
24*Kisha wakamwita mara ya pili yule mtu aliyekuwa ni kipofu, wakamwambia: Mtukuze Mungu! Sisi twajua: Mtu huyo ni mkosaji.#Yos. 7:19. 25Yule akajibu: Kama ni mkosaji, sijui; ninalolijua, ni hili moja: Mimi niliyekuwa kipofu naona sasa. 26Walipomwuliza: Amekufanyia nini? Amekufumbua macho jinsi gani? 27akawajibu: Nimekwisha kuwaambia; nanyi hamkusikia. Mnatakaje kuvisikia tena? Au nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake? 28Wakamtukana, wakasema: Wewe ndiwe mwanafunzi wake yule, lakini sisi tu wanafunzi wake Mose. 29Sisi tunajua, ya kuwa Mungu alisema na Mose, lakini huyo hatumjui, alikotoka. 30Yule mtu akajibu, akawaambia: Neno hili ni la kustaajabu, ya kuwa ninyi hamjui, alikotoka, naye amenifumbua macho! 31Twajua, ya kuwa Mungu hasikii wakosaji; ila mtu akimwogopa Mungu na kuyafanya, ayatakayo, basi, huyo humsikia.#Fano. 15:29; Yes. 1:15. 32Tangu hapo kale haijasikiwa, ya kuwa mtu aliyafumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu. 33Huyo kama angekuwa hakutoka kwa Mungu, asingeweza kufanya kitu.#Yoh. 9:16. 34Wakajibu, wakamwambia: Wewe uliyezaliwa wote mzima mwenye makosa, unatufundisha sisi? Wakamfukuza, atoke.#Yoh. 9:2.
35Kisha Yesu akasikia, ya kuwa wamemfukuza, atoke; alipomwona akasema: Unamtegemea Mwana wa mtu? 36Yule akajibu, akasema: Ni yupi, Bwana, nipate kumtegemea? 37Yesu akamwambia: Umekwisha kumwona, naye anayesema na wewe ndiye.#Yoh. 4:26. 38Ndipo, aliposema: Nakutegemea, Bwana! Akamwangukia. 39Kisha Yesu akasema: Nimekuja katika ulimwengu huu, niuhukumu, wasioona wapate kuona nao waonao wapate kupofuka.#Mat. 13:11-15. 40Wengine wao Mafariseo waliokuwa pamoja naye walipoyasikia haya wakamwambia: Je? Nasi tu vipofu?#Mat. 15:14; 23:26. 41Yesu akawaambia: Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa wenye makosa. Lakini sasa mkisema: Twaona, basi, makosa yenu yanawakalia.*#Fano. 26:12.
Iliyochaguliwa sasa
Yohana 9: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.