Alipokwisha kuyasema haya akaita na kupaza sauti: Lazaro, toka nje! Ndipo, yule aliyekufa alipotoka nje hivyo, alivyokuwa amefungwa kwa sanda miguu na mikono, nao uso wake ulikuwa umefunikwa kwa mharuma. Yesu akawaambia: Mfungueni, mmwache, aende zake!