Yohana 16
16
1Haya nimewaambia, maana msije kukwazwa.#Yoh. 14:29. 2Watawakataza kuziingia nyumba za kuombea; kweli saa inakuja, kila mwenye kuwaua ninyi atakapodhani, ya kuwa anamtumikia Mungu.#Mat. 24:9. 3Hivyo watavifanya, kwa sababu hawakumtambua Baba wala mimi.#Yoh. 15:21. 4Lakini nimewaambia haya, kwamba saa yao itakapokuja, myakumbuke, ya kuwa mimi nimewaambia ninyi. Lakini tangu mwanzo sikuwaambia haya kwa hivyo, nilivyokuwa pamoja nanyi.*
Kazi ya mtuliza mioyo.
5*Lakini sasa nakwenda kwake yeye aliyenituma, tena kwenu hakuna anayeniuliza: Unakwenda wapi?#Yoh. 7:33. 6Ila kwa sababu nimewaambia haya, mioyo yenu imejaa masikitiko. 7Lakini mimi nawaambiani lililo la kweli: Inawafalia, mimi niende zangu. Kwani nisipokwenda zangu, mtuliza mioyo hatawajia. Lakini nitakapokwenda, nitamtuma kwenu.#Yoh. 14:16,26. 8Naye atakapokuja atawaumbua wao wa ulimwengu kuwa wenye makosa wasio nalo la kujikania, wanaopaswa na kuhukumiwa.#1 Kor. 14:24. 9Ndio wenye makosa, kwa kuwa hawanitegemei mimi;#Yoh. 3:18; 15:22,24. 10hawana la kujikania, kwa kuwa nakwenda kwa Baba, nanyi hamnioni tena;#Tume. 5:31; Rom. 4:25; 1 Petr. 3:18. 11wapaswa na kuhukumiwa, kwa kuwa mtawala ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.#Yoh. 12:31; 14:30.
12Yako maneno mengi bado, ninayotaka kuwaambia; lakini sasa mngeyaona kuwa mzigo usiochukulika.#1 Kor. 3:1. 13Lakini yule atakapokuja, yule Roho wa kweli, yeye atawaongoza, awapeleke penye yote yaliyo ya kweli. Kwani hatayasema maneno yake mwenyewe, ila atayasema, atakayoyasikia, awatangazie nayo yatakayokuja.#Yoh. 14:26; 1 Yoh. 2:27. 14Yeye ndiye atakayenitukuza, kwani katika yale yaliyo yangu ndimo, atakamoyatwaa, atakayowatangazia ninyi. 15Yote, Baba aliyo nayo, ni yangu; kwa hiyo nilisema: Katika yale yaliyo yangu ndimo, atakamoyatwaa, atakayowatangazia ninyi.*#Yoh. 17:10.
Bado kidogo.
16*Bado kidogo hamtaniona; tena patakapopita kitambo kidogo, mtaniona tena, kwa sababu ninakwenda kwa Baba.#Yoh. 14:19. 17Basi, kulikuwako wanafunzi wake waliosemezana wao kwa wao: Neno hili, analotuambia, ni neno gani la kwamba: Bado kidogo hamtaniona, tena patakapopita kidogo, mtaniona? Na tena: Ninakwenda kwa Baba? 18Wakasema: Lile bado kidogo, alisemalo, ni kusemaje? Hatujui, analosema. 19Kwa kuwatambua, ya kuwa walitaka kumwuliza, Yesu akawaambia: Mnaulizana kwa hilo, nililolisema: Bado kidogo hamtaniona; tena patakapopita kidogo, mtaniona? 20Kweli kweli nawaambiani: Ninyi mtalia na kuomboleza, lakini wao wa ulimwengu watafurahi. Ninyi mtasikitika, lakini sikitiko lenu litageuka kuwa furaha. 21Mwanamke anapozaa husikitika, kwani saa yake imekuja; lakini akiisha kumzaa mwana hayakumbuki tena maumivu, ila hufurahi kwa ajili ya mtu aliyezaliwa kukaa ulimwenguni.#Yes. 26:17. 22Basi, nanyi sasa mnasikitika, lakini tutaonana tena, ndipo, mioyo yenu itakapofurahi; hiyo furaha yenu hakuna atakayeiondoa kwenu. 23Siku ile hamtaniuliza neno.*
*Kweli kweli nawaambiani: Lo lote, mtakalomwomba Baba, atawapa katika Jina langu.#Yoh. 14:20; 14:13-14. 24Mpaka leo hakuna, mliloliomba katika Jina langu. Ombeni! Ndipo, mtakapopewa, furaha yenu iwe imetimizwa yote!#Yoh. 15:11.
25Haya nimewaambia kwa mifano. Lakini saa inakuja, itakapokuwa, nisiseme nanyi tena kwa mifano, ila nitawatolea waziwazi mambo ya Baba. 26Siku ile mtaomba katika Jina langu, nani siwaambii: Mimi nitawaombea ninyi kwake Baba. 27Kwani Baba mwenyewe anawapenda, kwa sababu ninyi mmenipenda mimi na kunitegemea kwamba: Mimi nimetoka kwa Baba.#Yoh. 14:21. 28Nimetoka kwa Baba, nikaingia ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu, niende kwa Baba. 29Ndipo, wanafunzi wake waliposema: Tazama, sasa unasema waziwazi, usiseme mfano wo wote.#Yoh. 16:25. 30Sasa tunajua, ya kuwa unayajua yote, ya kuwa huulizwi na mtu. Kwa hiyo tunakutegemea, ya kuwa umetoka kwa Mungu. 31Yesu akawajibu: Sasa mnanitegemea? 32Tazameni, saa inakuja, tena imekwisha fika, mtawanyike kila mtu na kwao kwenyewe, mniache mimi, niwe peke yangu. Lakini mimi sipo peke yangu, kwani Baba yupo pamoja nami.#Yoh. 8:29; Mat. 26:31; Mar. 14:27; Zak. 13:7. 33Haya nimewaambia, mpate kutengemana mwangu. Ulimwenguni mnayo maumivu; lakini tulieni mioyo! Mimi nimeushinda ulimwengu.*#Yoh. 14:27; Rom. 5:1; 1 Yoh. 5:4.
Iliyochaguliwa sasa
Yohana 16: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
![None](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2F58%2Fhttps%3A%2F%2Fweb-assets.youversion.com%2Fapp-icons%2Fsw.png&w=128&q=75)
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.