Yohana 17
17
Maombo ya Yesu.
1Yesu alipokwisha kuyasema haya akayaelekeza macho yake mbinguni, akasema: Baba, saa imekwisha fika. Mtukuze Mwana wako, Mwana wako naye akutukuze! 2Ni kama hivyo, ulivyompa kumtawala kila mwenye mwili, awape wote, uliompa, uzima wa kale na kale.#Mat. 11:27. 3Nao huu ndio uzima wa kale na kale, wakutambue wewe, kwamba ndiwe peke yako Mungu wa kweli, tena wamtambue yule, uliyemtuma, kwamba ndiye Yesu Kristo.#Hos. 6:6; 1 Yoh. 4:8; 5:20. 4Mimi nimekutukuza nchini na kuitimiza kazi, uliyonipa ya kuifanya. 5Sasa, Baba, unitukuze kwako wewe na kunipa utukufu, niliokuwa nao nilipokuwa kwako, ulimwengu ulipokuwa haujawa bado.#Yoh. 1:1; 17:24; Fil. 2:6.
Kuwaombea wanafunzi.
6Jina lako nimewafumbulia watu, ulionipa na kuwatoa ulimwenguni. Walikuwa wako, nawe umenipa mimi, nalo Neno lako wamelishika.#Yoh. 17:9. 7Sasa wametambua, ya kuwa yote, uliyonipa, yametoka kwako. 8Kwani yale maneno, uliyonipa, nimewapa, wakayapokea, wakatambua kweli, ya kuwa nilitoka kwako, wakanitegemea, ya kuwa wewe ndiwe uliyenituma.#Yoh. 16:30. 9Mimi nawaombea hao, siuombei ulimwengu, ila nawaombea wale tu, ulionipa, kwani ni wako.#Yoh. 6:37,44. 10Nayo yote yaliyo yangu ni yako, nayo yaliyo yako ni yangu; namo mwao ndimo, nilimotukuzwa.#Yoh. 16:15. 11Nami simo tena ulimwenguni, lakini wao wamo ulimwenguni, kwani mimi nakuja kwako. Baba Mtakatifu, walinde, wakae na Jina lako, ulilonipa, wapate kuwa mmoja wote, kama sisi tulivyo mmoja!#Yoh. 10:30. 12Nilipokuwa pamoja nao naliwalinda, wakae na Jina lako, ulilonipa, nikawaangalia. Nao hawakuangamia hata mmoja wao, pasipo yule mwana wa mwangamizo, yaliyoandikwa yapate kutimia.#Yoh. 6:39; Sh. 41:10; 109:8. 13Lakini kwa kuwa sasa nakuja kwako, nayasema haya ulimwenguni, waipate furaha yangu, iwajie yote.#Yoh. 15:11. 14Mimi nimewapa Neno lako, ulimwengu ukawachukia, kwa sababu wao sio wa ulimwengu, kama mimi nisivyokuwa wa ulimwengu.#Yoh. 6:63. 15Siombi, uwaondoe ulimwenguni, ila naomba, uwalinde, yule Mbaya asiwajie.#Luk. 22:31-32; 2 Tes. 3:3. 16Wao sio wa ulimwengu, kama mimi nisivyokuwa wa ulimwengu. 17Watakase, wawe wa kweli! Neno lako ndilo la kweli.#Yoh. 6:63. 18Kama wewe ulivyonituma kwenda ulimwenguni, ndivyo nami nilivyowatuma kwenda ulimwenguni.#Yoh. 20:21. 19Nao ndio, ninaojitakasia mwenyewe, kwamba nao wawe watu waliotakaswa kweli.#Ebr. 10:10.
Kuwaombea Wakristo wote.
20Lakini si hawa tu, ninaowaombea, ila nawaombea hata wale watakaonitegemea wakilisikia neno lao. 21Wote wapate kuwa mmoja, kama ulivyomo mwangu, wewe Baba, nami nilivyomo mwako! Wapate kuwamo mwetu nao hao, ulimwengu upate kunitegemea, ya kuwa wewe umenituma.#Gal. 3:28. 22Nami nimewapa utukufu, ulionipa wewe, wapate kuwa mmoja, kama sisi tulivyo mmoja.#Tume. 4:32. 23Mimi niwemo mwao, nawe wewe uwemo mwangu, wawe watu waliomaliza kuwa mmoja, nao ulimwengu utambue, ya kuwa wewe umenituma, kisha umewapenda, kama ulivyonipenda mimi.#1 Kor. 6:17. 24Baba, nataka hata wale, ulionipa, wawe pamoja nami papo hapo, nitakapokuwapo mimi, wapate kuuona utukufu wangu, ulionipa, kwa sababu umenipenda, ulimwengu ulipokuwa haujaumbwa bado.#Yoh. 12:26. 25Baba mwongofu, ulimwengu haukukutambua, lakini mimi nimekutambua, nao hao wametambua, ya kuwa wewe umenituma. 26Nami nimewatambulisha Jina lako, na tena nitalitambulisha, kwamba upendo, wewe ulionipenda, uwakalie, nami niwemo mwao.
Iliyochaguliwa sasa
Yohana 17: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
![None](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2F58%2Fhttps%3A%2F%2Fweb-assets.youversion.com%2Fapp-icons%2Fsw.png&w=128&q=75)
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.