Yohana 7
7
Yesu na ndugu zake.
1Kisha Yesu alitembea huko Galilea, kwani hakutaka kutembea katika nchi ya Yudea, kwa kuwa Wayuda walitaka kumwua.#Yoh. 6:1. 2Lakini sikukuu ya Wayuda iitwayo ya Vibanda ilikuwa karibu.#3 Mose 23:34. 3Ndugu zake wakamwambia: Ondoka hapa, uende Yudea, wanafunzi wako nao wapate kuyaona matendo yako, unayoyafanya!#Yoh. 2:12; Mat. 12:46; Tume. 1:14. 4Kwani hakuna anayefanya kitu na kujifichaficha akitaka kujulikana waziwazi. Ukifanya hivyo watokee walimwengu, wakujue! 5Kwani hata ndugu zake hawajamtegemea. 6Kwa hiyo Yesu akawaambia: Siku zangu hazijafika bado; lakini siku zenu ziko siku zote.#Yoh. 2:4. 7Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, lakini mimi hunichukia, kwani naushuhudia, ya kuwa matendo yake ni mabaya.#Yoh. 15:18. 8Ipandieni ninyi sikukuu hii! Mimi siipandii bado sikukuu hii, kwani siku yangu haijatimia. 9Alipokwisha kuwaambia hivyo, akasalia Galilea.
10Lakini ndugu zake walipokwisha kuipandia sikukuu, ndipo, naye alipopanda; lakini hakutokea wazi, alikuwa kama mtu anayejifichaficha. 11Wayuda walimtafuta penye sikukuu, wakasema: Yuko wapi yule? 12Kukawa na manung'uniko mengi katika makundi ya watu kwa sababu yake. Wengine walisema: Ni mtu mwema; wengine walisema: Sio, ila hupoteza watu tu. 13Lakini hapana aliyemsemea mbele ya watu, kwa sababu waliwaogopa Wayuda.#Yoh. 9:22; 12:42; 19:38.
Yesu anafundishia Patakatifu.
14Lakini siku za katikati za sikukuu Yesu akapanda kupaingia Patakatifu, akafundisha. 15Wayuda walipostaajabu wakisema: Huyu anajuaje Maandiko, naye hakufundishwa?#Mat. 13:54. 16Yesu akawajibu, akasema: Mafundisho yangu siyo yangu, ni yake yeye aliyenituma. 17Mtu akitaka kuyafanya mapenzi yake yeye, atayatambua mafundisho haya, kama yametoka kwake yeye Mungu, au kama nayasema maneno yangu. 18Mwenye kuyasema yake hutafuta, atukuzwe yeye mwenyewe; lakini mwenye kutafuta, aliyemtuma atukuzwe, huyo ni mtu wa kweli, upotovu wo wote haumo moyoni mwake.#Yoh. 5:41,44. 19Siye Mose aliyewapa Maonyo? Tena kwenu hakuna mtu anayeyafanya Maonyo. Mnatafutiani kuniua?#Yoh. 5:16,18; Tume. 7:53; Rom. 2:17-24. 20Watu wakajibu: Una pepo! Yuko nani anayetaka kukuua?#Yoh. 5:16-18; 8:48,52; 10:20. 21Yesu akajibu, akawaambia: Ni tendo moja tu, nililolifanya, nanyi nyote mkalistaajabu.#Yoh. 5:16. 22Kwa sababu hiyo Mose aliwaagiza kutahiri watu; tena siye Mose aliyeviagiza, ila baba zenu. Nanyi humtahiri mtu hata siku ya mapumziko.#1 Mose 17:10-12. 23Mtu akitahiriwa siku ya mapumziko, kwamba Maonyo ya Mose yasivunjwe, mbona mnanikasirikia mimi, kwa sababu nimeponya mwili wote wa mtu siku ya mapumziko? 24Msiumbue kwa hivyo tu, mnavyoviona, ila umbueni maumbufu yapasayo!
Wakuu wanajaribu kumkamata Yesu.
25Palikuwa na wenyeji wa Yerusalemu waliosema: Si huyu, wanayemtafuta kumwua?#Yoh. 7:19. 26Tazameni, anasema waziwazi, wasimjibu neno! Labda nao wakubwa wetu wametambua kweli, ya kuwa huyu ni Kristo? 27Lakini huyu tunamjua, anakotoka; lakini Kristo atakapokuja, hakuna atakayetambua, atokako.#Yoh. 7:41; Ebr. 7:3. 28Ndipo, Yesu alipopaza sauti hapo alipofundishia Patakatifu, akasema: Mimi mnanijua, tena mnakujua, nilikotoka. Lakini sikujileta mwenyewe tu, ila yuko mwenye kweli aliyenituma, msiyemjua ninyi. 29Mimi ninamjua, kwani nimetoka kwake, naye amenituma.#Mat. 11:27. 30Walipojaribu kumkamata, hata mmoja hakumnyoshea mkono, kwani saa yake ilikuwa haijafika.#Yoh. 8:20; Luk. 22:53.
31Lakini wengi waliokuwamo kundini mwa watu wakamtegemea, wakasema: Kristo atakapokuja atafanya vielekezo vingi kuliko hivyo, alivyovifanya huyu?#Yoh. 8:30. 32Mafariseo waliposikia, watu wakinong'onezana hayo mambo yake, ndipo, watambikaji wakuu na Mafariseo walipotuma watumishi, wamkamate.
33*Yesu akasema: Nipo pamoja nanyi bado kidogo; kisha nitarudi kwake yeye aliyenituma.#Yoh. 13:33. 34Mtanitafuta, msinione; napo hapo, nitakapokuwapo, ninyi hamwezi kupafika.#Yoh. 8:21. 35Ndipo, Wayuda waliposema wao kwa wao: Huyu anataka kwenda wapi, sisi tusimwone? Atawaendea wale waliotawanyika kwa Wagriki, awafundishe Wagriki? 36Ni neno gani hilo, alilolisema: Mtanitafuta, msinione? Napo hapo, nitakapokuwapo, ninyi hamwezi kupafika?
Mito ya maji ya uzima.
37Siku ya mwisho iliyokuwa kubwa katika sikukuu Yesu alikuwa amesimama, akapaza sauti akisema: Mtu akiwa na kiu na aje kwangu, anywe!#Yoh. 4:10; 3 Mose 23:36; Yes. 55:1. 38Mwenye kunitegemea, kama yalivyoandikwa, mwilini mwake yeye mtatoka mito ya maji yenye uzima.#Yes. 44:3; Yoe. 2:28. 39Hivyo alisema kwa ajili ya Roho, watakayepewa waliomtegemea; kwani Roho alikuwa hajaonekana bado, kwa sababu Yesu alikuwa hajaupata utukufu wake.*#Yoh. 16:7. 40Wengine waliokuwamo kundini mwa watu walipoyasikia maneno hayo wakasema: Huyu ndiye kweli yule mfumbuaji.#Yoh. 6:14; 5 Mose 18:15. 41Wengine wakasema: Huyu ndiye Kristo, wengine wakasema: Je? Kristo atatoka Galilea?#Yoh. 1:46. 42Je? Andiko halikusema: Kristo atatoka katika uzao wa Dawidi mle kijijini mwa Beti-Lehemu, alimokaa Dawidi?#2 Sam. 7:12; Mika 5:1; Mat. 2:5-6; 22:42. 43Basi, watu wakakosana kwa ajili yake.#Yoh. 9:16. 44Wenzao wengine walitaka kumkamata, lakini hakuna aliyemnyoshea mikono.#Yoh. 7:30.
45Kisha wale watumishi wakarudi kwa watambikaji wakuu na kwa Mafariseo; nao walipowauliza: Mbona hamkumleta? 46watumishi wakajibu: Tangu kale mtu hajasema hivyo kama mtu huyo anavyosema.#Mat. 7:28-29. 47Mafariseo wakawajibu: Nanyi mmepotezwa? 48Je? Yuko mkubwa au Fariseo anayemtegemea? 49Ni hili kundi la watu tu wasioyatambua Maonyo, ndio walioapizwa. 50Ndipo, Nikodemo aliyemjia siku zile usiku, aliyekuwa mmoja wao, alipowaambia:#Yoh. 3:1-2. 51Maonyo yetu huhukumu mtu, asiposikiwa kwanza, yatambulikane aliyoyatenda?#5 Mose 1:16-17. 52Wakajibu, wakamwambia: Je? Nawe u mtu wa Galilea? Tafuta, uone, ya kuwa hakuna mfumbuaji anayetoka huko Galilea!#Yoh. 7:41. 53Wakaenda zao kila mmoja nyumbani kwake.
Iliyochaguliwa sasa
Yohana 7: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.