Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo 15:36-41

Matendo 15:36-41 BHN

Baada ya siku kadhaa, Paulo alimwambia Barnaba, “Turudi tukawatembelee wale ndugu katika kila mji tulikolihubiri neno la Bwana, tukajionee jinsi wanavyoendelea.” Barnaba alitaka wamchukue pia Yohane aitwaye Marko. Lakini Paulo hakupendelea kumchukua Marko, ambaye awali aliwaacha kule Pamfulia na kukataa kushiriki katika kazi yao. Basi, kukatokea ubishi mkali kati yao, wakaachana. Barnaba akamchukua Marko, wakapanda meli kwenda Kupro. Naye Paulo akamchagua Sila, na baada ya ndugu wa mahali hapo kumweka chini ya ulinzi wa neema ya Bwana, akaondoka. Katika safari hiyo alipitia Siria na Kilikia, akiyaimarisha makanisa.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Matendo 15:36-41