Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 12

12
Kuomba msaada
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo wa Sheminithi. Zaburi ya Daudi)
1Fanya haraka, ee Mwenyezi-Mungu!
Watu wema wamekwisha;
waaminifu wametoweka miongoni mwa watu.
2Kila mmoja humdanganya mwenzake,
husema kwa kudanganya na kwa moyo wa unafiki.
3Ee Mwenyezi-Mungu
uikomeshe hiyo midomo ya udanganyifu,
na ndimi hizo zinazojigamba kupindukia.
4Wao husema: “Kwa ndimi zetu tutashinda;
midomo tunayo, nani awezaye kututawala?”
5Lakini Mwenyezi-Mungu asema:
“Kwa sababu maskini wanadhulumiwa,
na wahitaji wanapiga kite, sasa naja,
nami nitawapa usalama wanaoutazamia.”
6Neno la Mwenyezi-Mungu ni safi,
safi kama fedha iliyosafishwa katika tanuri,
naam, kama fedha iliyosafishwa mara saba.
7Utulinde, ee Mwenyezi-Mungu,
utukinge daima na kizazi hiki kiovu.
8Waovu wanazunguka kila mahali;
upotovu unatukuzwa kati ya watu.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 12: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia