Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 14:1-7

Zaburi 14:1-7 BHN

Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu.” Wote wamepotoka kabisa, wametenda mambo ya kuchukiza; hakuna hata mmoja atendaye jema! Mwenyezi-Mungu anawaangalia wanadamu kutoka mbinguni, aone kama kuna yeyote mwenye busara, kama kuna yeyote anayemtafuta Mungu. Lakini wote wamekosa, wote wamepotoka pamoja; hakuna atendaye mema, hakuna hata mmoja. “Je, hao watendao maovu hawana akili? Wanawatafuna watu wangu kama mikate; wala hawanijali mimi Mwenyezi-Mungu.” Hapo watashikwa na hofu kubwa, maana Mungu yu pamoja na waadilifu. Unaweza kuvuruga mipango ya maskini, lakini Mwenyezi-Mungu ndiye kimbilio lake. Laiti ukombozi wa Israeli ungefika kutoka Siyoni! Mwenyezi-Mungu atakaporekebisha hali ya watu wake, wazawa wa Yakobo watashangilia; Waisraeli watafurahi.

Soma Zaburi 14